CHINI MFUNGAJI WA TIMU YA MZINGA REHEMA KASSAM AKIJIANDAA KUFUNGA GOLI HUKU AKIWA AMEZONGWA NA WACHEZAJI WA TUPENDANE YA MKOANI LINDI WAKATI WA MASHINDANO HAO YA NETIBOLI TAIFA.
MCHEZAJI WA TUPENDANE LINDI ZUHURA KASSIM KULIA AKIMILIKI MPIRA DHIDI YA LUCY THOMAS WA TIMU YA MZINGA MOROGORO WAKATI WA MASHINDANO HAYO.
MASHINDANO ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli yameanza kutimua vumbi kwa timu mwenyeji ya Alliance One kupokea kipigo katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya timu ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya kwa kupoteza kwa kufungwa bao 31 kwa 17 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mchezo huo walinzi wa timu ya Hamambe waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Alliance One katika mchezo huo huku wageni hao wakitawala sehemu ya kiungo na kuzidisha mashambulizi dhidi ya wapinzani wao.
Hamambe ilionyesha dalili za ushindi mapema baada ya kipindi cha kwanza kuweza kutumbukiza mabao 16 dhidi ya mabao 6 ya Alliance One huku mabao ya Hamabe yakifungwa kwa ushirikiano na washambuliaji Martha William na Subira Ally wakati ya Alliance One yakitumbukizwa katika nyavu na Vida Mengo na Mariam Juma na hadi kipindi cha kwnza kinamalizika kufanya matokeo kuwa 31 kwa 17.
Katika pindi cha pili Hamambe iliweza kufunga mabao 16 huku timu ya Alliance One iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na kufanikiwa kufunga 11.
Wakati mchezo wa kwanza wa ufunguzi ukimalizika kwa wenyeji kupoteza mchezo huo dhidi ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya kwa bao 31 kwa 17 timu ya JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ilicheza mchezo wa pili kwa kuonyeshana kazi na akinadada wa Kurugenzi Tandahimba na kuwashushia kichapo cha bao 40 kwa 20.
Kikosi cha kocha mkuu wa timu ya JKT Ruvu Argentina Daudi kilionyesha nia ya kutaka kutwaa ubingwa huo na panda ligi daraja la kwanza msimu ujao kwa kuwang’uta bila huruma timu ya Kurugenzi Tandahimba kutoka mkoani Mtwara baada ya wafungaji wenye uchu wa bao Jawa Iddi kufunga bao 32 huku Ashura Sadiki akifunga mabao 8.
Timu ya Kurugenzi Tandahimba iliweza kupata mabao kupitia kwa washambuliaji wake Nasra Seleman na Magreth Mrekoni kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa JKT Ruvu 40 na Kurugenzi Tandahimba kuambulia 20.
Katika mfululizo wa mashindano yao yanayaoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa ilichezwa michezo mingine kwa timu nne kushuka dimbani kutafuta pointi kwa timu ya Polisi Pwani kuonyeshana kazi na timu ya Kurugenzi Ruangwa kutoka mkoa wa Lindi kumalizika kwa Polisi Pwani kuibuka na ushindi wa bao 26 kwa 22 ya Ruangwa.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa upinzani mkali kipindi cha kwanza Polisi Pwani waliweza kuongoza kwa bao 10 dhidi ya mabao 9 ya Ruangwa ambapo timu hizo zilionyesha kiwango cha juu katika kiopindi cha kwanza hadi kinamalizika.
Kipindi cha pili kiungo wa timu ya Polisi Pwani Gaudencia Cliton alifanya kazi ya ziada ya kuhahakisha anatafuta mipira kila kona ya uwanja na kutoka pasi za mwisho kwa washambuliaji wake ili kuweza kufunga kwa urahisi.
Washambuliaji wa timu ya Polisi Pwani, Fatuma Ahmed na Pasifika Salanga walitumia udhaifu wa walinzi wa Kurugenzi Ruangwa ambao walimezidi ujanja kwa kushindwa kuwakaba ipasavyo na kutoa mwanya washambuliaji hao hasa katika kipindi cha pili kufunga mabao hao 26 huku Ruangwa wakiambulia bao 22 yaliyofungwa na Amina Mussa na Naima Ramadhani.
Timu ya Polisi Arusha iliweza kuisambaratisha timu ya akinadada wa Tigo kutoka kudni B baada ya kuwaendesha mchakachamka na kuwafungwa bao 25 kwa 15 wakati timu mwenyeji ya Mzinga nayo ilianza vema michuano hiyo baada ya kuwatandika timu ya Tupenda kutoka mkoa wa Lindi kwa bao 25 kwa 13.
Katika mchezo huo wenyeji timu ya Mzinga iliweza kupata mabao hayo kupitia kwa washambuliaji Jamilla Sabu na Rehema Kassamu katika katika mchezo mungine wa kundi B JKT Ruvu iliweza iliweza kuwapigisha kwata ndugu zao wa Black Sisters ya Kibaha zote za mkoa wa Pwani kwa kuzifunga mabao 47 dhidi ya 10.
JKT Ruvu ambayo ilitawala kila idara ya mchezo huo iliweza kuwadhibiti ndugu zao hao kwa kipindi cha kwa kuwafunga mabao 23 mabao yaliyofungwa na Jawa Iddi aliyefunga jumla ya bao 26 huku Ashura Sadiki akifunga bao 21 wakati mabao ya Black Sisters yalifungwa na Kemmy Seleman 3 na Farida Juma akifunga bao 7.
Mashindano hayo yaendelea mchana huu katika kundi A kwa kuzikutanisha timu za Kurugenzi Ruangwa na Alliance Onne huku Hamambe ikionyeshana kazi na Mzinga wakati kundi B Polisi Arusha itacheza NA Tandahimba na Black Sisters ya Kibaha kutoka mkoa wa Pwani dhidi ya Tigo katika uwanja huo huo wa Jamhuri mkoani Morogoro.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment