MANAHODHA MORO ALL STAR NA BONGO FLAVA
MWAMUZI WA MAPAMBANO LA MCHEZO WA SOKA HAMISI KAMBI WA PILI KUTOKA KUSHOTO AKIJADILIANA JAMBO NA MANAHODHA TUNDA MAN WA BONGO FLAVA WA KWANZA KULIA NA WA PILI YEKE NI PROFESA MADUNDO MTAMBO WA MORO ALL STAR KABLA YA KUANZA KWA MCHEZO HUO KATIKA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO WENGINE WASAIDIZI WA MCHEZO HUO.
TIMU ya soka ya Bongo Flova Fc imepoteza mchezo wake dhidi ya timu ya soka ya Moro All Stars kwa kukubali kipigo katika mchezo wa soka wa kuchangia fedha kwa ajili ya wahanga wa mabomu wa Gongo la Mboto ya Jijini Dar es Salaam uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa bao 3-1.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani mkali kwa kila timu na kutandaza soka safi ambapo huku wakishangiliwa na mashabiki wao ilikuwa timu ya Bongo Fleva Fc ndiyo ilianza mchezo kwa kulifikia lango la wapinzania wao kwa kumjaribu kipa wa timu ya Moro All Star, Bule Mtagwa katika dakika ya kwanza pale mshambuliaji tegemeo Alli Kiba alipopiga mpira kimo cha mbuzi akiwa nje ya 18 na mpira huo kutoka setimita chache kutoka langoni la mwapinzania wao katika cmhezo huo.
Nayo timu ya Moro All Star iliwachukua dakika ya 12 kuweza kupachika bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Meck Meckcime aliyefunga bao la kuongoza baada ya kufanya kazi ya ziada ya kuwalamba chenga mabeki wa Bongo Flava Fc kabla ya kupiga mpira uliokwenda wavuni na kumwacha mlinda mlango timu hiyo ya Bongo Flava Tunda Man kuukondolea macho mpira ukitinga wavuni na asijue la kufanya na kuandikia timu ya Moro All Star bao la kuongoza katika mchezo huo uliohudhuliwa na mashabiki wengi waliokaa katika majukwaa kaatika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Baada ya kupata bao hilo la kuongoza timu ya Moro All Star ilizidisha mashambulizi kwenye lango la wapinzania wao na katika dakika 16 kupitia kwa mshambuliaji wao Profesa Madundo Mtambo aliangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Bongo Flava Fc Tunda Man na mwamuzi wa kati Hamis Kambi kutoa adhabu ya penalti iliyopigwa kiufundi na kiungo wa timu hiyo Ashraf Pedo na kuandika bao la pili katika kipindi hicho cha kwanza na kwenda mapumziko Moro All Star ikitoka kifua mbele kwa bao 2-0.
Timu ya Bongo Flava Fc ilipata bao lao la kufutia machozi lililofungwa na mshambuliaji wao tegemeo Alli Kiba kwa njia ya penalti katika dakika ya 36 baada ya mshambuliaji wa Bongo Flava Fc na beki wa Moro All Star ambapo mwamuzi Hamisi Kambi alitoa adhabu ya penalti na kupata bao hilo la kufutia machezo katika mchezo huo.
Katika mchezo huo mwamuzi Hamis Kambi aliweza kuwapa kadi ya njano wachezaji Dominic Mbawala wa Moro All Star na mlinda mlango wa Bongo Flava Fc Tunda Man kutokana na mchezo mbaya.
Timu ya Moro All Star baada ya timu ya Bongo Flava Fc kupata bao la kwanza iliendeleza kufanya mashambulizi mfululizo katika lango la wapinzania wao na katika dakika ya 89 ilifanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na mshambuliaji Dominc Mbwala na kuufanya mchezo huo timu ya Bongo Flava Fc kupoteza kwa kukubali kipigo kutoka kwa timu ya Moro All Star kwa bao 3-1.
0 comments:
Post a Comment