MKUU wa mkoa wa Morogoro Issa Machibya amenusuriki kifo baada ya gari lake ambalo alikuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la kwa Mnyonge barabara ya zamani ya Old Dae se Salaama baada ya kugonga mti wakati dereva wa gari hiyo akimkwepa mwendesha pikipiki asimgonge kabla ya kuachia njia na kuingia katika mashamaba ya mpunga mjini hapa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea majira ya saa 11 alasiri machi 15 ilihusisha na pikipiki yenye namba ya usajili T734 BMK Sunlg na gari la mkuu huo ambalo lilikuwa likiendesha na dereva Abeid Namangasa (43) wakati ikitokea Bigwa kuelekea mjini ambapo ghala mwendesha pikipiki aliyetambuliwa kwa jina la Edwin Rugambwa (33) mkazzi wa Kichangani Morogoro baada ya kudaiwa kubadilisha mwelekeo wakati akitoka mjini na kuelekea eneo la Bigwa.
Akizungumza na gazeti hili katika eneo la tukio dereva wa gari la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Abeid Namangasa (43) alisema kuwa ajali iliyotokea baina ya gari la na pikipiki imesababishwa na mwendasha pikipiki baada ya kubadilisha mwelekea ghafu kwa kukata kona na kurudi alikotoka mjini na wakati huo gari yake tayari ilikuwa ipo jirani naye na kulazimika kumkwepa ili nisimgonge.
Namangasa alisema baada ya kuona mwendesha pikipiki amebadilisha ghafla mwelekeo kwa kukata kona na kurudi alikotoka ililazimika amkwepe ili asije asimgonge mtu huyo na kutembea pembeni mwa barabara lakini baadaye aliona mwelekeo wake mbele kuna ngema kubwa na kuinghiza pembeni na kugonga mti wa mwembe kabla ya kusimama umbali wa mita 50 kutoka barabarani katika mashamaaba ya mpunga katika eneo hilo la Kwa Mnyonge.
Baada ya kutokea tukio hilo mwendesha pikipiki aliweza kuroka eneo la ajali na kukimbia lakini baadaye aliweza kukamatwa na kuelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mpanda pikipiki kwa kubadilisha mwelekeo ghafla na kusababisha kutokea kwa uharibifu wa gari hilo la mkuu wa mkoa wa huo.
Athibitisha kwa kutokea kwa ajali Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Adolfina Chialo alisema kuwa machi 15 majira ya saa 11 alasiri katika eneo la Kwa Mnyonge barabara ya Old Dar es Salaam kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro gari lenye namba ya usajili SKT 6601 toyota Land Cruiser S/Wagon mali ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro ilipata ajaili wakati ikitokea Bigwa na kuelekea mjini ikiendesha na dereva Abeid Namangasa iligonga mti wakati ikimkwepa mwendesha pilipiki ili isimgonge.
Kamanda Chialo alisema katika ajali hiyo ambayo imehusisha gari la mkuu huyo na pikipiki yenye namba ya usajili T734 BMK Sunlg iliyokuwa ikiendeshwa na Edwin Rugambwa (33) mkazzi wa Kichangani Morogoro akieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mpanda pikipiki kwa kubadilisha mwelekeo ghafla na kusababisha kutokea kwa ajali na baada ya kutokea kwa tukio hilo alikimbia lakini jeshi la polisi lilimkamata na kuweka chini ya ulinzi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment