BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANNE WATUHUMIWA KWA UJANGILI KATIKA HIFADHI YA WANYAMAPOLI YA WAMI-MBIKI

WATU wanne wanaodaiwa kuwa ni majangili wamekamatwa katika hifadhi ya wanyama poli ya Wami-Mbiki baada ya kukutwa na nyama ya wanyama aina ya Tandala na Kongoni ndani ya hifadhi hiyo katika eneo la Kisanda kata ya Ubena Zomozi wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kufikishwa kwa watuhumiwa hao wanne wa ujangili katika ofisi za hifadhi ya Wami-Mbiki mkoani Morogoro Mkuu wa Msafari wa maaskari wa doria Joseph Dominic alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na kuona nyayo za watu katika eneo la Kisanda majira ya saa moja na nusu usiku ya machi 14 mwaka huu wakati wakiwa katika doria ndani ya hifadhi hiyo.

Dominic alisema baada ya kuona nyayo hizo ilitulazimu kulala eneo hilo na asubuhi tulianza kazi ya kufuatilia mwelekeo wa nyayo hizo zikijikita zaidi ndani ya hifadhi hiyo na baada ya kutembea umbali wa kilometa tatu tuliona watu wanne wakianika nyama na kuwavamia na kuwaweka chini ya ulinzi.

“zile nyayo baada ya kuziona tulilala eneo lile la Kisanda kwa sababu usiku tayari ulishafika na asubuhi tulianza kufuatilia mwelekeo wa nyayo zile ambazo zilijikita zaidi ndani ya hifadhi na tulipotembea umbali wa kilometa tatu tuliona watu wanne wakiwa na nyama kavu ya wanyama waliowaua aina ya Tandala na Kongoni lakini na tuliwavamia na kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi wetu. Alisema Dominic.

Mkuu huyo alisema kuwa mara baada ya kuwakamata watu hao Omari Saidi (73) Almasi Athmani (49), Juma Jaeka (49) na Bakari Mustafa wote wakazi wa kijiji cha Viskaza kata ya Ubena Zomozi wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani waliwahoji juu ya bunduki baada ya kuona maganda matatu ya bunduki ya short gun ilitumika kuwaua wanyama na kuhoji iko wapi hiyo bunduki na kuelezwa kuwa bunduki wanayo wenzao wawili ambao wakati huo walikuwa mtoni kwa ajili ya kuchota maji kwa ajili ya kusongea uji kwa madai kuwa mwanzao mmoja alikuwa akisumbuliwa na tumbo na matumizi mengine ya watuhumiwa hao wa ujangili.

Askari hao waliwafutilia wale wenzao wawili ambao walidai walielekea mtoni kwa ajili ya kuchota maji lakini walipofika mtoni hawakuweza kuwakuta na kugundua kuwa wametoroka katika eneo lile la tukio ambapo waliwabeba watuhumiwa hao wanne na kuelekea katika ofisi kuu ya hifadhi hiyo mkoani Morogoro. Alisema Dominic.

Aidha akiongea na mwandishi wa gazeti hili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Wami-Mbiki mjini hapa mmoja wa watuhumiwa hao Almasi Athmani mkazi wa kijiji cha Visaza kitongoji cha Lukwambe wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani akielezea juu ya tukio hilo alisema kuwa machi 14 walifuatwa kwa nyakati tofauti na Saidi Omari na kuwaeeleza kuwa wakamsaidie kubeba mzigo eneo la Kisanda na wao walikubaliana naye juu ya ombi lake hilo.

Athmani alisema kuwa baada ya kukubali ombi la Saidi Omari la wamsaidia kubeba mzigo katika eneo la Kisanda ambapo walifika na kubaini kuwa mzigo wenyewe ni nyama poli na walianza kazi ya kutayarisha kwa kuweka katika viroba na majira ya saa nne ya machi 15 walivamiwa na askari wa wanyama poli wa hifadhi ya Wami-Mbiki na kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi wao.

“tulivamiwa na askari wa wanyma poli majira ya saa nne asubuhi machi 15 wakati tukitayarisha nyama tukiiweka katika viroba na kutukamata na kuweka chini ya ulinzi lakini jambo la kwanza watuuliza bunduki tuliyotumia kuua wanyama iko wapi na tuliwajibu kuwa bunduku hiyo anayo Saidi Omari ambaye yupo mtoni kuchota maji na huyo ndiye mhusika mkuu sie tumeitwa tu kubeba mzigo wao na kuona mazungumzo yetu na sakari walitumia mwaya huo kutoroka, alisema Almasi.

Pia Athmani alisema katika mahijiano kuomba viongozi wakuu wa hifadhi ya Wami-Mbiki wawasemehe kwa kuwapiga faini ya sh laki moja (100,000) ili kuwaachia huru waendelee na maisha ya kilimo kwani walibaini kuwa Saidi Omari alikuwa amewadanganya na kuwaingiza katika matatizo makubwa ya kuingia ndani ya hifadhi ya wanyama poli bila kujua.

Naye Kaimu Meneja wa Hifadhi ya Wami-Mbiki Abubakari Msonde ametoa wito kwa wananchi wanaoishi kwa kuzunguka katika hifadhi hiyo kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazo wawezesha kukamata watu wanaojihusisha na mali za mazao ya hifadhi hiyo kwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyo karibu nao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: