BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHUO CHA ARDHI MOROGORO CHAFANIKIWA KUPIMA VINJWA 4200 KATIKA MIKOA NANE KWA MWAKA 2010.

WAHITIMU WA CHUO CHA ARDHI MOROGORO KUTOKA VERONICA GEORGE, ADAM MWIGUNE NA ANGEL MESS WAKIWA NA VYETI VYAO MARA BAADA YA KUHITIMU KOZI YA UPIMAJI ARDHI KATIKA MAHAFALI YA 29 YALIYOFANYIKA CHUONI HAP.



MMOJA WA WAHITIMU WA KOZI YA UPIMAJI ARDHI SWAUMU MBEGU AKIFURAHIA JAMBO MARA BAADA YA KUKABIDHIWA NA MGENI RASMI AMBAYE NI KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MARIA BILIA WAKATI WA MAHAFALI YA 29 YA CHUO HICHO CHA ARDHI MOROGORO.


CHUO cha Ardhi mkoa wa Morogoro kupitia watalaamu wake kimefanikiwa kupima jumla ya viwanja 4200 vya makazi na matumizi mbalimbali katika mikoa nane ikiwa ni harakati za kuboresha huduma za makazi kwa mwaka 2010 hapa nchini.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro, Deusderius Kimbe alisema jumla ya viwanja 4200 vimepimwa katika mpango maalum kupitia wataalam wa chuo hicho katika mikoa nane hapa nchini lengo likiwa ni kutekeleza sera ya serikali na kutoa huduma kwa wananchi ya kuboresha makazi katika mfumo ulio sahihi.

Kimbe alisema kuwa licha ya kupima viwanja katika maeneo hayo pia chuo hicho kilishiriki kikamilifu katika kupima viwanja zaidi ya 2000 kwa waadhirika wa mafuriko katika wilaya ya Kilosa mwaka huo 2010.

Kaimu huyo wa Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro alitaja maeneo ambayo watalaam wa chuo hicho kupima viwanja kuwa ni katika mkoa wa Arusha eneo la ya Bulka na Lakilaki ikiwa na jumla ya viwanja 1600 vilivyopimwa, mkoa wa Dodoma katika wilaya za Kondoa viwanja 400, Bahi viwnja 50 na mji wa Mpwapwa viwanja 300 na mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo viwanja 120.

Alitaja mikoa mingine kuwa ni mkoa wa Iringa katika wilaya ya Njombe viwanja 300 na mkoa wa Morogoro katika wilaya za Mvomero viwanja 872 eneo la Dakawa Sokine pamoja na Manispaa ya Morogoro viwanja 480. Alisema Kimbe.

Aidha Kimbe alisema kuwa chuo cha ardhi mkoa wa Morogoro kina uwezo wa kupima viwanja 10,000 hadi 15,000 endapo serikali inaweza kuwawezesha fedha za ghalama za kazi hiyo hapa nchini kwa mwaka.

Pia ametoa wito kwa wananchi, Halmashauri, makampuni na wadau wa ardhi kuendeelea kukiamini na kukitumia chuo hicho cha ardhi Morogoro ili kuendelea kuwatumia wataalam na kufaidika na elimu waliyoipata chuoni hapo.

Chuo cha ardhi Morogoro kilianishwa mwaka 1978 kikiwa kama tawi la kilichokuwa chuo kikuu cha Ardha Dar es Salaam kikiwa na lengo la kuandaa wataalam wa kubuni na kupima viwanja mijini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: