BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAMA na mtoto wamefariki dunia papo hapo huku abiria 30 wakijeruhiwa baada ya basi waliokuwa wakisafiria la kampuni ya Al Saedy kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam kupata ajali iliyohushwa na lori na kupinduka eneo la Sangasanga kwa Mwarabu katika wilaya ya Mvomero barabara kuu ya Iringa-Morogoro mkoani hapa.


Ajali hiyo ambayo ilitokea Majira ya 11:45 jioni april 22 mwaka huu katika eneo hilo basi lenye namba ya usajili T 267 AWG Scania mali ya kampuni ya Al Saedy yenye makao makuu mkoani Morogoro ilikuwa inaendeshwa na dereva Erick Luoga ikitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam iligongana na lori lenye namba ya usajili T 346 ABX Scania likiwa na tela T 657 AGU mali ya kampuni ya Trans Cargo ya Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na dreva, Ally Khamis (48) mkazi wa Kigogo Jijini Dar es Salaam ilisababisha vifo vya abiria wawili mama na mtoto wake katika ajali hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkuu wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwakamaku alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:45 jioni barabara kuu Iringa-Morogoro eneo la Sangasanga kwa Mwarabu wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baada ya lori lenye namba ya usajili T 346 ABX Scania likiwa na tela T 657 AGU kuligonga basi hilo na tele wakati akiwa katika harakati za kupishana na kusabisha dereva wa basi la Al Saedy kuyumba kabla ya kuacha njia na kupinduka na kisha kusababisha watu wawili mama na mtoto kufariki dunia papo hapo na abiria 30 kujeruhiwa.


Mwamakula alisema abiria hao ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo bado hawajatambuliwa kwa majina huku majeruhi wanaume wakiwa 18 na wanawake 12 na walikimbizwa katika hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu zaidi.


Mkuu huyo wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro aliwataja majeruhi wa basi hilo la kampuni ya Al Saedy kuwa ni Flotela Hiyela (20) mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, Matilda Nyenze (23) mkazi wa Soweto mkoani Mbeya, Ubaya Zahoro ambaye ni askari magereza mkoa wa Pwani, Francis Kizinga (50) bohari wa Mwakareli sekondari ya Tukutu Mbeya, Benjamini Nywage (20) mkazi wa Tabata Dar es Salaam na Martin Charles (18) mwanafunzi wa sekondari ya Mbalizi mkazi wa Tabata Dar es Salaam.


Aliwataja wengine kuwa ni Amelina Msungu (47) mkazi wa Mjipya Morogoro, Ester Rajab (21) mkazi wa Uyole Mbeya, Witness Juma (20) mkazi wa Vingunguti Dar es Salaam, Atu Mlembe (13) mkazi wa Kilosa Iringa, Alafisa Mwipopo (56) mkazi wa Mufindi Iringa, Salum Thabit (31) Imambi Mbeya, Joseph Paul (35) mkazi Tegeta Dar es Salaam, Maneno Idha (20) mkazi wa Morogoro, Mwanaheri Mogera (20) Mlangali Mbeya, Rose Mwakatobe (42) mkazi wa Ilomba Mbeya, Raison Kalulunga, Baheto Bwerera (52), Fikiri Zuberi mkazi wa mkazi wa Modeko Morogoro na Oscar Kidili mkazi wa Uzunguni Mbeya.


Mwamakula alisema kuwa dereva wa lori lililosaabaisha ajali hiyo ambaye alikuwa kielekea Iringa alijisalimisha katika kituo kidogo cha polisi cha Doma mkoani hapa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: