MASHINDANO ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISETA) yameanza kutimua vumbi kwa kushirkisha michezo mbalimbali ambapo michezo hiyo imegawanywa kwenye kanda sita April 11 mwaka huu ndani ya Manispaa ya Morogoro mjini hapa.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini hapa Mratibu wa mashindano hayo, Redmayne Mwandisi alisema mashindano hayo yameanza kutimua vumbi april 11 mwaka huu katika viwanja sita tofauti ambapo timu zimegawanywa kutokana na makundi ya kanda hizo sita.
Mwandisi alitaja michezo ambayo wachezaji wanashiriki kuwani mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, netiboli, basketball, mpira wa wavu, bao na riadha.
Kwa upande wa kanda alitaja kanda hizo ambazo zitachezwa michezo hiyo kuwa ni mjini kati yenye jumla ya timu saba, kanda ya Sua ambayo ina timu sita, kanda ya Bigwa yenye timu saba na kanda ya Tungi na yenye jumla ya timu saba.
Alitaja kanda nyingine kuwa ni Kihonda A ambayo ina timu nane na kanda ya Kihonda B ambayo yenyewe ina jumla ya timu sita.
Aidha Redmayne alisema kuwa katika kila kanda hizo sita timu shiriki zitacheza katika mfumo wa ligi na mshindi wa kwanza ataungana na washindi wengine ambapo watacheza na kutafuta bingwa wa mashindano hayo.
“haya mashindano tumeyagawanya katika kanda sita na kila kanda zitacheza na zitatafuta mshindi wake ambapo kila mshindi wa kwanza kutoka kwenye kanda hizo watakutana na kucheza ligi ambayo atapatikana bingwa wake”. Alisema Redmayne.
Lengo la mashindano hayo ni kutafuta vipaji kutoka kwenye timu zinazoshiriki na baada ya kupata wachezaji tutaunda timu ya wilaya ya Morogoro ya umiseta ambayo itachiriki mashindano ya mkoa huo. Alisema Mratibu huyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment