ABOOD AZINDUA BENKI YA WANANCHI VIJIJINI (VIKOBA) YA NGOTO A MORO.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki ya wananchi vijijini (VIKOBA) ya Ngoto A kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoroeneo la Masika, wa pili kutoka kushoto ni Diwni wa kata hiyo Mohamed Lukwele.
MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood ametoa wito kwa benki za wananchi vijijini (VIKOBA) kuongeza juhudi za kuingiza wanachama wengi kwani vikundi hivyo vimekuwa suluhisho la kutatua matatizo mbalimbali katika jamii ya vikundi hivyo mkoani hapa.
Akizungumza katika uzinduzi wa kikundi cha Ngoto A kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro Abood alisema kuwa benki za wananchi vijijini zikisimamiwa vizuri na viongozi pamoja na kuongeza idadi kubwa ya wananchama suala ya umakisini kwa mwanancham moja moja wa vikundi hivyo litapungua kwa jiasi kikubwa.
Abood alisema kuwa ipo haja kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujiunga na vikundi mbalimbali vilivyopo katika kata zote 29 za Manispaa hiyo kwani utafiti umeonyesha kusaidia wanachama wake na jamii inayozunguka katika matatizo mbalimbali.
“nimetembelea vikundi hivi karibu vikundi 15 vya Manispaa yetu na kuelezwa kuwa malengo makubwa ni kusaidiana katika matatizo ya kijamii ikiwemo msiba, ulipaji wa ada ya wanafunzi shuleni, kutoa ajira kwa vijana sasa malengo ya vikundi hivi ni mazuri” alisema Abood.
Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Ngoto A, Salum Ally alisema kuwa kikundi hicho kina aina tatu za uchangiaji ikiwemo mfuko wa maendeleo wa jamii, hisa na kutoa mikopo kwa wanachama ambapo mwanakikundi hurejesha fedha katika kikundi kwa liba ya 5% ya fedha anazokopo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kikundi hicho kina jumla ya wanachama 33 wanaume wakiwa 14 na wanawake 19.
Katika Manispaa ya Morogoro ina jumla ya benki za wananchi vijijini 220 (VIKOBA) katika kata zake 29 na inakadiriwa kuwa na wananchama zaidi ya 500.
0 comments:
Post a Comment