VIFAA vyenye thamani ya Sh 15Mil vimekabidhiwa kwa viongozi wa timu nne zinazoshiriki mashindano ya Taifa Cup katika kituo cha Morogoro na wadhamini wa mashindano hayo TBL kwa mwaka 2011 mjini hapa.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa timu hizo nne zinashiriki mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Issa Machibya alisema katika mashindano hayo anatarajia kuona wanamichezo kucheza mchezo mzuri utaowavutia mashabiki na kutoa sapoti ya kuwashangia kutokana na imana aliyonayo ya kuona vipaji vipya vikijitokeza katika mashindano hayo.
Machibya alisema kuwa baadhi ya wachezaji wameshindwa kuonyesha vipaji vyao kutokana na kukosa kuonyesha vipaji katika mashindano mengine makubwa hapa nchini hivyo nafasi hiyo waitumie vizuri kwa kuonyesha ujuzi wao katika mchezo huo wa soka ambao unapendwa na mashabiki wengi duniani.
Mkuu huyo alisema anatoa pongezi kwa kamati ya maandalizi ya shirikisho la michezo nchini TTF kukipatia kituo mkoa wa Morogoro ya mashindano hayo ya taifa Cup mwaka 2011 na kuwa hatua imekuwa tunu kwa wakazi wa mkoa wa huo na mashabiki wa mchezo huo wa soka kupata fursa ya kuangalia michuano hiyo.
Naye Mkuu wa kituo cha mashindano hayo kutoka TBL Willie Marthin alitaja vifaa vilivyotolewa na mdhamini kuwa ni jezi pea mbili, mipira kumi, tracksuit tano kwa viongozi wa timu pamoja na malazi na chakula vyote vikiwa na thamani ya sh 15Mili.
Alisema kuwa kila timu imepata vifaa hivyo ambazo zinashiriki mashindano na kuwa wataendelea kutoa pea za vifaa katika hatua ya robo fainali kwa timu zitakazo fuzu hatua hiyo huku katika kila mchezo atachaguliwa mchezaji bora wa mchezo na kukabidhiwa kiasi cha sh 100,000 mara baada ya mchezo kumalizika.
Katika mashindano hayo timu ya mkoa wa Morogoro Moro Stars itafungua dimba kwa kucheza na timu ya mkoa wa kisoka wa Ilala majira ya saa 8 mchana kesho
jumamosi katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment