BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UMITASHUMTA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO JAMHURI

MKUU wa wilaya ya Mvomero Fatuma Mwassa anatarajia kufungua mashindano ya umoja wa michezo shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya mkoa wa Morogoro ambayo itashirikisha timu sita za michezo za wilaya za mkoa huo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa leo.

Akizungumza na gazeti hili katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa Afisa Michezo wa Manispaa ya Morogoro, Asteria Mwang’ombe alisema kuwa mkuu wa wilaya ya Mvomero wilaya ya Mvomero anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya Umitashumta ngazi ya mkoa wa huo ambayo yatayoanza kutimua vumbi juni 11 majira ya saa 8 mchana kwa michezo ya mpira wa miguu na netiboli kwenye uwanja huo.

Mwang’ombe alisema kuwa licha ya kuwepo kwa michezo hiyo ya ufunguzi katika michezo ya soka wavuana na netiboli kwa wasichana pia kutakuwa na mchezo maalum wa soka kwa walemavu wa kusikia (viziwi) kati ya shule ya msingi Kilakala kitengo cha viziwi na wenzao wa kitengo cha viziwi shule ya msingi Kiwanja cha Ndege katika ufunguzi huo.

Alisema kuwa katika mashindano hayo wilaya sita za mkoa wa huo tayari zimewasili katika Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya michuano hiyo ikiwemo wilaya ya Kilosa, Mvomero, Ulanga, Morogoro Vijijini, Kilombero na mwenyeji Morogoro Manispaa ambapo washiriki watashindana katika mbio za riadha kuanzia mita 100 hadi mita 3000, mpira wa wavu wavulana na wasichana, kurusha mitupo na kuruka pamoja na taaluma katika darasa la tatu hadi darasa la sita.

Pia Mwang’ombe ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Jamhuri katika mashindano hayo ili kuweza kuona vipaji vya watoto wao katika michezo hiyo.

Mashindano hayo yatatumika katika kuteua wachezaji mbalimbali kwa ajili ya kuunda timu za michezo tofauti katika mkoa huo wa Morogoro ambayo itashiriki mashindano ya kanda ya mashariki yatayofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: