MAJERUHI AJALI YA BASI LA HOOD NA LORI WAPATIWA MSAADA WA MADAWA YETHE THAMANI YA SH 2.1 MIL.
MMOJA WA MAJERUHI WALIOPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM KWA AJILI MATIBABU ZAIDI HAPO AKIWA WARDI NO 1 YA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO KABLA YA KUONDOKA.
MADAWA yenye thamani ya sh 2.1Mil yametolewa msaada na wafadhili mbalimbali kwa majeruhi wa ajali ya basi la hood na lori katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na abiria watano kufariki dunia na 41 kujeruhiwa iliyotokea julai 20 mwaka huu katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Mikumi mkoani hapa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Frida Mokiti alisema kuwa amepokea madawa yenye thamani ya sh 2,120,000 mil yaliyotoewa na wafadhili mbalimbali baada ya kutokea kwa ajali hiyo julai 20 mwaka huu.
Aliwataja walitoa msaada wa madawa hayo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya mabasi ya hood Mohamed Hood aliyetoa kiasi cha sh 240,000 na juice, mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood aliyetoa madawa yenye thamani ya 1,400,000 na Jitu Raseru aliyetoa madawa yakiwa na thamani ya 480,000.
Akizungumzia juu ya hali ya majeruhi wa ajali hiyo Dk Mokiti alisema kuwa majeruhi sita kati ya 41 waliopelekwa katika hospitali ya mkoa huo wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Aliwataja majeruhi waliopelekwa katika hospitali ya rufaa kuwa ni Benito mkazi wa Arusha, James Shitindi mkazi wa Arusha, dereva wa basi hilo la hood Saleh Tembo mkazi wa jijini Dar es Salaam, Peter Jemimo mkazi wa Kibaha mkoani Pwani, Charles Jesaya mkazi wa Singida na mtoto Joyce Kamkanila (11).
Alisema kwa sasa hospitali ya mkoa wa Morogoro ina wajeruhi 10 ambao wanaaendelea vizuri na kupatiwa huduma huku wengine 25 wakiwa wameruhusiwa kwenda majumbani kwao.
Aidha mganga huo alisema kuwa hospitali ya mkoa wa Morogoro inakabiliwa na uhaba wa madawa kutokana na bajeti iliyotengewa ukilinganisha na mahitaji.
0 comments:
Post a Comment