BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KIPIGO KOCHA MKUU WA YANGA SAM TIMBE ATAKA WACHEZAJI KUJITUMA

KOCHA Mkuu wa Yanga Sam Timbe amewataka wachezaji wa klabu yake kujituma zaidi ili kuweza kutetea ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuanza vibaya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu JKT kwa kupoteza kwa kuruhusu bao 1-0 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.


Timbe alisema kuwa kupoteza kwa mchezo huo kumetokana na wachezaji kushindwa kujituma na kudai kuwa safu ya ushambuliaji nayo imeshindwa kutekeleza majukumu yao kwa kushindwa kutumia vema nafasi walizopata wakiwa katika nafasi nzuri ya kufunga ambapo hali hiyo imewanufaisha wapinzani wao katika mchezo huo kwa kuibuka na pointi tatu.

Alisema safu ya ushambuliaji ya timu yake imeshindwa kutumia vema nafasi walizopata kufunga na kuwataka kujituma katika mchezo ujao dhidi ya Moro United ambao utafanyika jumatano agosti 24 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.


“safu ya ushambuljia imeniangusha kutokana na kushindwa kupatachika mabao kwani katika mchezo ule sisi tulicheza kipindi cha pili na hawa wapinzani wetu walicheza vizuri kipindi cha kwanza na tumeshindwa kutumia vema nafasi tulizopata” alisema Timbe.


Timbe alisema kuwa kwa sasa analifanyia kazi hasa safu ya ushambuliaji kwa kuongeza mbinu ya mbalimbali za ufungaji katika mazoezi ambayo hali hiyo hatarajia kujitokeza tena katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri ikiwa ni maandalizi kwa mchezo na Moro United.


Akizungumzia juu ya yeye kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Jamhuri Timbe alisema waandishi wa habari za michezo amewaomba waandae utaratibu nzuri wa kutafuta namna ya kuongea na makocha mara baada ya kumalizika kwa mchezo kwa kutafuta eneo maalum la kuongea na makocha tofauti na hali iliyopo sasa ambapo mwaandishi unaongea na makocha sehemu yo yote ambapo hali hiyo sio nzuri kiusalama.


Alisema utaratibu huo ni nzuri kama itaandaliwa sehemu maalum ya makocha kuzungumzia mchezo ambapo alishauri kutenga eneo mojawapo la uwanja huo wa Jamhuri aidha kwa kushilikiana na wafanyakazi wa uwanja huo au jeshi la polisi ili iwe rahisi kwao kutoa tathimini ya mchezo husika.


“mimi sikugoma kuongea na waandishi wa habari nilichotaka ni kuwepo kwa chumba cha mikutano sasa ninyi waandishi mkishindwa kufanya hilo basi mshirikiana na jeshi la polisi kuwepo na ulinzi lakini ni mara baada ya kuondoka kwa mashabiki kwani mashabiki wamekuwa na tabia ya jazba mara baada ya timu zao kupoteza mchezo kwani kiusalama suala hilo sio sahihi” alisema Timbe.

Timbe alisema kuwa mashabiki wanapaswa kufahamu hakuna kiongozi anayependa timu ipoteze mchezo kwani wamekuwa na jazba hasa timu yao inapofanya vibaya hivyo hiyo inakuwa ni hatari kwao makocha kuzungumza wakati bado mashaki wapo ndani ya uwanja huku wakiwa na jazba hari inayo hofu kuwa wanaweza kufanya jambo lolote baya kutokana na timu yao kupoteza mchezo.


Kocha huyo amewataka mashabiki wa klabu ya Yanga kutulia kwani jopo zima la ufundi wanalifanyia kazi baada ya kupoteza mchezo huo ili mchezo ujao wafanye vizuri.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: