TAASISI isiyo ya kiserikali ya Islamic Foundotion ya Morogoro imeadhimisha kilele cha sikukuu ya Idd El Fitri kwa kufanya tamasha la Idd El Fitri kwa michezo mbalimbali huku Rajabu Ndivati na Ramadhan Feruzi wakiibuka washindi wa kwanza katika mbio za baiskeli iliyoshirikisha wapanda baiskeli 15 na kuibuka na zawadi ya pesa taslim sh 40,000 katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Akizungumza na BLOGU hili mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo Mratibu wa tamasha hilo Mohamed Matano alisema kuwa Rajabu Ndivati ameibuka mshindi wa kwanza katika mbio za baiskeli za kilometa 25 zilizoanzia msikiti wa Karume na kumalizikia uwanja wa Jamhuri huku kwa upande wa walemavu Ramadhan Feruzi aliibuka mshindi wa kwanza kwa kuwaongoza wanzake kuzunguka uwanja wa Jamhuri mara tano katika wapanda baiskeli 10 na kila moja akipata zawadi ya sh 40,000.
Matano alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwakusanya waumini wa dini ya kiislam kujumujika pamoja kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa ramadhani kwa waumini wa dini ya kiislam ambapo iliwashirikisha wakazi wa mikoa mitatu ya Pwani, Dar es Salaam na wenyewe Morogoro ambapo zaidi ya michezo saba washiriki walishirki katika katika michezo hiyo katika tamasha hilo ambalo liliwajumuisha zaidi ya waumini 2500 kutoka mikoa hiyo.
Alitaja michezo mingine kuwa ni mchezo wa soka ambao kulikiwa na timu nne za Young Muslim, timu ya mchanganyika ya mkoa wa Pwani, timu ya chuo kikuu cha kiislam na timu ya viongozi wa taasisi hiyo ya Islamic Foundotion ya Morogoro.
Matano alisema katika mchezo huo wa soka timu ya viongozi wa Islamic Foundotion ya Morogoro iliibuka kidedea baada ya kuilaza timu ya mchanganyiko ya Pwani kwa kuilaza bao 1-0 lililofungwa na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Nahdi Aref kwa njia ya penalti katika dakika ya 15 baada ya beki wa Pwani Swafa Nabahani kufanya madhambi katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Ramadhan Mtoro kutoa adhabu hiyo.
Ushindi huo ni mara baada ya timu ya Chuo kikuu cha kiislam Morogoro kutoa sare ya bao 1-1 na Young Muslim na kuwapa nafasi ya timu ya viongozi wa Islamic Foundotion kuibuka mabingwa katika tamasha hilo ambalo lilihudhuliwa na mamia ya waumini wa dini hiyo ya kiislam katika uwanja huo wa jamhuri Morogoro.
Alisema kuwa katika tamasha hilo lililoshirikisha rika mbalimbali kulikuwa na michezo mingine ikiwemo kukimbia na magunia, kufukuza kuku, kupanda farasi, mbio fupi za mita 100 kwa watoto na watoto kushindana kula andazi katika kamba ambapo katika kufukuza kuku mshindi aliondoka na kuku huyo kwa ajili ya kitoweo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WAIBUKA NA ZAWADI YA SH 40,000 KATIKA TAMASHA LA MICHEZO LA ISLAMIC MORO KILELE CHA SIKUU YA IDD EL FITRI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment