Kiongozi wa chama kinachofuata siasa za wastani za mrengo wa shoto, PDP, ambacho kilionekana kuwa kitachukua nafasi ya pili kabla ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasi nchini Tunisia , amekubali kushindwa leo wakati kura zikiendelea kuhesabiwa. Kiongozi wa chama cha PDP Maya Jbril ameliambia shirika la habari la AFP katika makao makuu ya chama hicho kuwa mwelekeo unajulikana, na chama cha PDP hakiko katika nafasi nzuri, na huu ni uamuzi wa watu wa Tunisia. Maya ameyasema hayo wakati chama kinachofuata nadharia za dini ya Kiislamu cha Ennahda kimedai kuwa kinaongoza.
Tume huru ya uchaguzi haijatoa matokeo yoyote, lakini mjumbe wa baraza kuu la chama cha Ennahda , Ali Marayedh, ameliambia shirika la habari la Ujerumani kuwa matokeo ya mwanzo yanakiweka chama hicho mbele kabisa. Vyama 77 vimeweka orodha ya wagombea katika uchaguzi wa Jumapili kuwania viti 217 katika bunge la nchi hiyo ambalo litakuwa na wajibu wa kuunda katiba mpya na kuteua serikali ya muda. Kwa mujibu wa kiongozi wa tume ya uchaguzi, Kamal Jendoubi , idadi ya watu waliopiga kura katika uchaguzi wa jana Jumapili imefikia asilimia 70.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment