BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Maiti ya Gaddafi yakaguliwa.

Afisa anayechunguza vifo vya ghafula nchini Libya atakagua mwili wa Kanali Gaddafi hii leo, huku maswala yakiendelea kuulizwa kuhusu vipi aliuwawa.

Maiti yake sasa iko katika chumba cha barafu (jokofu) cha kuweka nyama mjini Misrata - ikiwa na alama ya risasi kichwani.

Familia ya Kanali Gaddafi inataka maiti yake itolewe.

Lakini haijulikani atazikwa wapi.

Maafisa wa daraja za juu wa serikali ya mpito wamesema sherehe rasmi itafanywa kesho, kutangaza kuwa Libya imeshakombolewa yote.

Marekani na Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa Libya kufanya uchunguzi wa wazi juu ya kifo cha Kanali Gaddafi.

Kuna shaka kuwa aliuliwa kusudi, siyo kwa ajali, katika mapambano ya risasi, kama ilivoelezwa rasmi na wakuu wa Libya.

Maiti ya Gadaffi imewekwa katika chumba cha barafu (jokofu) cha kuweka nyama mjini Misrata.

Afisa mhusika anatarajiwa kukagua maiti hiyo kikamilifu hii leo.

Wananchi wa Libya wanapiga foleni kwenda kuona maiti ya kiongozi huyo wa zamani pamoja na mtoto wake, Mo'tassim, ambaye piya aliuwawa Alkhamisi.

Kila mtu anazungumza juu ya video iliyopigwa kwenye simu ya mkononi, inayoonesha dakika za mwisho za kiongozi huyo, kabla ya kufa.

Viongozi wa serikali ya muda ya Libya lazima waamue kama watamzika hadharani au watafanya maziko ya siri na haraka, kabla ya kutangaza ukombozi kamili wa Libya hapo kesho, na kutoa tarehe ya uchaguzi wa kidemokrasi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: