BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SMAL KIDS YAENDELEA KUSUASUA LIGI DARJA LA KWANZA TANZANIA BARA KUNDI B.

Mshambuliaji wa Smal Kids, Rmadhan Boimanda akimtoka mlinzi wa Majimaji ya Songea Mahmadu Wazigi wakati wa mchezo wao wa ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Majimaji ilishinda bao 3-0.


Mlindamlango wa Majimaji, Mzee Njala akinyanyua daruga juu mbele ya washambuliaji wa Smal Kids huku akidaka mpira wakati wa mchezo wao wa ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Majimaji ilishinda bao 3-0.


TIMU ya soka ya Smal Kids ya Rukwa imeendelea kusuasua katika ligi daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Majimaji ya Songea katika kundi B mchezo ambao uliowakutanisha na kutandikwa bao 3-0 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro juzi.

Mabao yote ya washindi yalipachikwa wavuni na mshambuliaji wa Majimaji, Peter Mapunda ambapo kipigo hiko kilitokana na safu ya ulinzi ya Smal Kids kushindwa kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao huku safu ya ushambuliaji nayo ikishindwa kutumia vema nafasi walizopata za kufunga na kusababisha timu hiyo kuambulia kipigo hicho cha ba0 3-0.

Kamwe benchi la ufundi la Smal Kids halitaweza kumsahau mashambuliaji hatari wa Majimaji, Peter Mapunda kutokana na kuihadaa ngome ya ulinzi na kuweza kufumania nyavu huku bao lake la kwanza akifunga dakika ya 43 kwa adhabu ndogo na mpira kwenda moja kwa moja wavuni kufuatia mlinzi wa Smal Kids kufanya madhambi nje kidogo ya eneo la hatari.

Katika dakika 64 mwamuzi wa mchezo huo, Saidi Issa kutoka Singida alimtoka nje ya uwanja, Henry Anthony wa Majimaji baada ya kumtwanga ngumi mchezaji wa Smal Kids na kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo.

Kuanza kwa kipindi cha pili Majimaji waliingia kwa kasi na kufanya mashambulizi katika lango la Smal Kids na dakika ya 59 na 75 kupitia mshambuliaji huyo, Peter Mapunda aliongeza mabao mawili, bao la pili akishirikiana vema na Shabil Issa huku la tatu akifunga baada ya mlinzi wa Smal Kids, Yusuf Malipili lililotokana na kuchanganyana na mlinda mlango wake, Mzee Njala kabla ya mfungaji kukwamisha mpira wavuni.

Timu hiyo ya Smal Kids ya Rukwa inayonolewa na kocha, John William (Dero Piero) ambayo kwa sasa imehamia uwanja wa nyumbani wa Jamhuri Morogoro imeteremka dimbani kucheza michezo mitatu ambapo katika mchezo wa kwanza ilitoa bao 0-0 dhidi Prison ya Mbeya na kutoa katika mchezo wa pili na JKT Mlale ya mkoani Songea ya bao 0-0 huku mchezo wa tatu ikiambulia kipigo cha bao 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea na kukusanya pointi mbili katika michezo hiyo mitatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: