WAKATI viongozi wa Taasisi ya Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), wakiendelea kusota mahakama kuu kwa tuhuma za kuendesha mchezo wa upatu, kanisa la Glory of Christ Assembles Church la kata ya Mazimbu manispaa ya Morogoro limepigwa mnada baada ya waumini wake kushindwa kulipa mkopo wa Sh 113 milioni za kampuni ya Tanzania Gatsby Trust (TGT) walizozipeleka DECI.
Hali hiyo imewafanya waumini wa kanisa hilo zaidi ya waumini 200 kushindwa kuabudu jumapili iliyopita kufuatia kanisa lao kuuzwa kwa njia ya mnada na kampuni hiyo kutokana na kanisa hilo kuwa dhamana ya mkopo huo.
Kanisa hilo lilikopa fedha hizo kutoka TGT, na kuzigawa kwa vikundi vya ujasiliamali vilivyoundwa na waumini wa kanisa hilo katika vipindi tofauti lakini vikundi hivyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati iliyo ilazimu kampuni hiyo kupiga mnada kanisa hilo.
Akitoa ufafanuzi wa sakata hilo mchungaji wa kanisa hilo, Eddy Lucas alililiambia Mwananchi kuwa fedha hizo zilikopwa na kanisa hilo mwaka 2008 na mwaka 2009 kiasi cha Sh 69.9, lakini kiwango hicho kiliongezeka kutokana na riba.
Mchungaji huyo aliongeza kuwa vikundi hivyo vyenye wanachama zaidi ya 104 vilikopeshwa fedha hizo mwezi Januari mwaka 2009 na marejesho yake yalitarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huo lakini yalishindikana kutokana na fedha zilizopelekwa DECI kushindwa kurejeshwa.
Alisema wengi wa wanachama wa vikundi hivyo waliochukua mikopo hiyo walizipeleka kwenye taasisi ya DECI ili kupanda mbegu na kuvuna zaidi jambo ambalo lilikuwa kinyume cha matarajio yao baada ya serikali kuifungia taasisi hiyo na viongozi wake kufikishwa mahakamani.
Mchungaji huyo alisisitiza kuwa lengo la kukopesha vikundi hivyo lilikuwa zuri kwani hiyo ilikuwa ni moja sera ya TGT, hivyo kanisa lake lilichukua jukumu la kuchukua mkopo kutoka katika kampuni hiyo na kisha kuvikopesha vikundi vya wajasiliamali vilivyoundwa na waumini wake.
Mchungaji Lucas alisema kuwa baada ya vikundi hivyo kushindwa kuresha fedha kwa wakati, kwa TGT kama makubaliano yalivyo kuwa na matokeo yake kusababisha deni hilo kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa riba hadi kufikia Sh43.1milioni ikiwemo gharama nyingine na kufanya kiwango cha fedha kinachodaiwa kufikia Sh113milioni.
Katika mnada huo mali ambazo ziliuzwa ni pamoja na kanisa, nyumba tatu na gari ndogo aina ya Toyota Corona vyote vikiwa vimeuzwa kwa thamani ya Sh39 milioni.
Alisema mnada huo uliendeshwa kwa kukiuka baadhi ya taratibu za kuendesha mnada uliosimamiwa na kampuni ya Tulvin Investment Company Ltd ya jijini Dar es Salaam ikiwemo kutoa tangazo la mnada siku mmoja na siku iliyofuatia shughuli za mnada ziliendeshwa jambo ambalo anadai analitilia shaka juu ya uuzaji wa mali za kanisa.
“Nimeshangazwa na mnada ulivyoendeshwa na Tulvin Investment Company Ltd ya Dar es Salaam kwa kutoa tangazo la mnada siku moja na siku iliyofuatia mnada kufanyika kwa ufahamu wangu unaponadisha mali kwa njia ya mnada tangazo hufanyika mwezi mmoja kabla ya siku ya kufanyika mnada, lakini hili imefanyika kwa hila kutokana na eneo hili limekumbwa na migogoro ya muda mrefu kati ya kanisa na baadhi ya kundi la watu wanaozunguka kanisa hilo” alisema Mchungaji Lucas.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tulvin Investment Company Ltd iliyoendesha mnada huo, Kelvin Samuel alisema katika mnada huo jumla ya sh 39milioni zilipatikana kutokana na uuzaji wa mali ikiwemo kanisa na nyumba tano lililouzwa kwa thamani ya Sh37milioni katika kitalu 479 na 480, gari ndogo aina ya Toyota Corona yenye namba za usajiri T 843 ACW kwa tahamni ya Sh 2milioni.
Samuel alisema kuwa kanisa hilo linadaiwa kiasi cha sh69.9milioni lakini kutokana na gharama za uendeshaji ikiwemo riba imefanya deni hilo kufikia Sh113milioni ambapo kwa sasa wanaangalia namna ya kukamata mali nyingine ili kuweza kupigwa mnada kufidia kiasi kilichobaki cha sh 74milioni kutokana na kupata kiasi cha Sh 39milioni.
Akizungumzia juu ya mgogoro uliopo kati ya kanisa hilo Glory of Christ Assembles Church Mazimbu, Mchungaji, Lucas alisema kumekuwa na mgogoro ulioanza mwaka 2001 kati ya pande hizo mbili huku wakazi wa jirani na eneo hilo wakilalamikia ibaada za usiku zinazoendeshwa na kanisa hilo ambazo huanza majira ya saa 3.00 usiku.
Mchungaji huyo alibainisha kuwa siku mmoja mtu asiyefahamika alifyatua mshale ndani ya kanisa hilo wakati ibaada ikiendelea lakini mshale huo ambao baadaye kwa taarifa za kipolisi ulibainika kuwa na sumu haukuweza kumdhuru mtu yeyote na kwamba hakuna mtu yeyote aliyakamatwa kushiriki tukio hilo.
“Nililengwa mshale wenye sumu wakati naendesha ibada usiku lakini bahati mzuri mshale ule haukumjeruhi mumini yoyote licha kulengwa mimi na kukita madhabahuni na tulipojaribu kutoka nje hatukumuona mtu yo yote na tuliuchukua mshale ule hadi polisi kule ndiko walikogundua kuwa ulikuwa na sumu” alisema Mchungaji Lucas.
Alisema mbali ya tukio hilo kumekuwa na mfululizo wa matukio ya hujuma katika kanisa hilo ambapo mwaka 2003 uongozi wa kanisa hilo uliitwa ofisi ya kata Mazimbu kujibu tuhuma zilizotolewa na baadhi ya kikundi kisicho julikana wakidai kuwa waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakipiga kelele nyakati za usiku wakati wa ibada zao na kushindwa kupata usungizi.
Aliendelea kutaja matukio yalifanyika kwa kusema kuwa Machi 19 mwaka 2011 gari ndogo lenye namba ya usajili T251 Suzuki Escudo ilichomwa moto na watu asiyefahamika majira ya usiku.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / KANISA LA GLORY OF CHRIST ASSEMBLES CHURCH LAUZWA KWA NJIA YA MNADA BAADA YA KUSHINDWA KULIPA DENI LA MKOPO WA SH113MILIONI MOROGORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment