MICHUANO YA CECAFA SENIOR CHALENGE CUP 2011.
Timu ya taifa ya Malawi imeisambaratisha timu ya taifa ya Kenya Harembee Stars 2–0 katika mchezo wa kundi C wa michuano ya Mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na kati CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP uliochezwa katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Bao la kwa la Malawi lilipatikana katika dakika ya 24 likifungwa na John Banda huku wakipata bao la pili kwa njia penati ilifungwa na Joseph Kamwend baada ya golikipa wa Harambee Stars Duncan Ochieng kumshika mchezaji mmoja wa Malawi ndani ya kumi na nane.
katika mchezo baina ya Sudan na Ethiopia ulimalizika kwa sare ya 1-1 katika mchezo wa kundi C. Goli la sudan lilifunguwa na Tahir Osman katika dakika ya tano ya kipindi cha kwanza.
Mechi nyingine iliyochezwa kundi B ambayo ilifanyika katika uwanja wa Azam nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam ambapo timu ya taifa ya Uganda The Cranes imeisambaratisha bila huruma timu ya taifa ya Somalia kwa jumla ya magoli 4 -0.
Emmanuel Okwi ambaye pia ni mshambuliaji wa Timu ya Simba ya Tanzania aliifungia timu yake ya Uganda hat trick yaani magoli matatu.
0 comments:
Post a Comment