Polisi duniani wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kujaribu kuwakamata wahalifu wanaosakwa, lakini hapa Uingereza polisi wamewaomba wezi wanaotafutwa kujisalimisha wenyewe na wakifanya hivyo watapatiwa bia za bure.
Polisi katika jimbo la Derbyshire wametoa fursa hiyo kwa kundi la washukiwa kadhaa, ambao wameahidiwa watapewa creti moja la bia kwa kila atakayejisalimisha.
Kampeni hiyo ya polisi inayojulikana kama Operation Rocky tayari imewavutia washikiwa kumi na tisa, ambao wamejisalimisha na kukata kiu zao za bia.
"Hawa ni wahalifu ambao wamekuwa wakiukimbia mkono wa sheria kwa muda mrefu, kwa hiyo tumeamua kutumia njia hii" amesema inspekta mkuu Graham McLaughlin. Washukiwa hao wanatafutwa kwa uhalifu wa wizi na kunyanyasa kijinsia.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment