Rwanda yarudisha madini Congo-Kinshasa
Rais Kagame wa Rwanda
Madini yasiopungua tani 82 yaliokamatwa na polisi wa Rwanda yanarudishwa Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ikiwa hizi ni dalili za kuimarika kwa uhusiano kati ya majirani hao wawili.
Madini hayo ni pamoja na yale ya cassiterite, bati na vile vile coltan, ambayo hutumiwa kujenga vifaa kama vile simu za mkononi.
Kurejeshwa vifaa hivyo kunafuatia sheria za kimataifa zinazonuiwa kusafisha sekta hiyo inayokabiliwa na ufisadi wa hali ya juu.
Utajiri wa madini wa Congo Kinshasa umekuwa kichocheo kikuu cha mzozo wa miaka mingi nchini humo.
Makundi ya watu wenye silaha kutoka nchini humo na nje wameyateka machimbo mengi upande wa mashariki, maeneo yanayopakaana na Rwanda na ni Rais wachache tu wa Congo ndio waliofaidika na utajiri huo mkubwa wa madini wa nchi yao.
Rwanda imeivamia mara mbili Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ikisema imekuwa ikipigana na makundi ya waasi yaliokuwa hapo, lakini jeshi lake limeshutumiwa kwa kupora madini wakati wa mzozo ambapo watu wanaokisiwa kuwa milioni tano waliuawa.
Mwandishi wa BBC Will Ross anasema kuwa shughuli ya kurejesha madini hayo mpakani ni dalili za kuonesha kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili ambazo zilikuwa maadui.
"Hili linadhihirisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili" mshauri wa wizara ya madini alisema haya alipozungumza na BBC.
Naibu mkurugenzi wa idara ya mali asili wa Rwanda Michael Biryabarema amesema Rwanda inataka kukomesha fikra kuwa ilifaidika kutokana na uchimbaji haramu wa madini katika jamhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Amesema kuwa Rwanda na Jamuhuri ya Kidemoctrasia ya Congo zitafanya kazi pamoja kuimarisha sekta zao wa maadini.
Rwanda kwa miaka mingi imekuwa ititajwa kuwa ilipora maadini kutoka Congo.
Ilikanusha hapo awali kuhusika na uporaji wowote lakini sasa inasaidia juhudi za kufanya biashara ya madini iwe na uwazi.
Madini yoyote yatakayokamatwa bila ya kuwa na alama yatarejeshwa alisema Bw.Biryabarema.
Mapema wiki hii kuna tovuti iliyoanzishwa kuimarisha uwazi katika sekta ya maadini Congo.
Kituo cha Carter Center kimesema kuwa tovuti hiyo www.congomines.org itawapa watu taarifa zaidi kuhusu sekta ya maadini ikiwa nipamoja na kandarasi na malipo.
Mamia ya nyaraka za maadini na ramani pia zitachapishwa katika wavuti hiyo.
Lakini taasisi kubwa ya serikali ya maadini Gecamines haitatoa taarifa kuhusu kandarasi zake bila ya kibali kutoka kwa wenzao wanaoshirikiana nao katika biashara hiyo, haya ni kwa mujibu wa mkuu wa taasisi hiyo Kalej Nkand.
0 comments:
Post a Comment