Wakati kampeni zikipamba moto Drc baadhi ya wanaharakati wanasema ni mabadiliko ya kisiasa pekee yatakayoleta amani katika ukanda huo.
Katika wiki za mwisho za kampeni huko Congo malori kama haya ya chama tawala yamekuwa na umaarufu mkubwa.
Mivutano na hamasa zinapanda juu Mashariki mwa DRC wakati wapiga kura wanapojiandaa kwa uchaguzi wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika jimbo liloharibiwa na vita la Kivu Kaskazini wanaofanya kampeni wamemimika mitaani na baadhi ya wanaharakati wanasema ni mabadiliko ya kisiasa pekee yatakayoleta amani katika ukanda huo.
Kwa wakati mmoja rais wa sasa Joseph Kabila alijivunia umashuruhi mkubwa katika jimbo hilo, lakini mitaa kadhaa kando na hapo, wafuasi wa mgombea urais , Vital Kamerhe, wamekusanyika nje ya makao makuu ya afisi zake za kampeni wakipunga mikono yao na kupaza sauti zao wakimuunga mkono bwana Kamerhe.
Bw. Kamerhe ni miongoni mwa wagombea watatu wakuu kati ya wagombea 11 wanowania kiti cha rais, na ni mashuhuri hasa huko eneo la mashariki. Uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika Novemba 28.
0 comments:
Post a Comment