BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Kabila atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi Kongo


Mahakama Kuu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imeidhinisha tangazo la tume ya uchaguzi nchini humo kuwa rais Joseph Kabila amechaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 mwezi uliopita.


Majaji wa mahakama hiyo iliyo katika mji mkuu Kinshasa wameyakataa matakwa ya upinzani kuwa matokeo hayo yafutiliwe mbali.

Mawakili wa mgombea aliyeibuka wa tatu katika kinyanganyiro hicho cha urais na spika wa zamani Vitalis Kamerhe, waliondoka mahakamani humo wakiueleza uamuzi huo wa mahakama kuwa "kinaya ya haki".

Mahakama hiyo iliamua kuwa Kabila ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 48.95 dhidi ya mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi aliyepata asilimia 32.33.

Wiki iliyopita Tshisekedi aliyakataa matokeo yaliyotangazwa hapo awali na alijitangaza kuwa rais wa taifa hilo, huku akitoa wito wa kuhifadhi utulivu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: