BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA SHIMIVUTA KUFIKIA TAMATI KESHO MORO.

Mlinzi wa timu ya soka ya chuo cha walimu Nyerere Kivukoni (MNMA) Charles Mashabara kulia akiondoa hatari kwa kupiga tik taka huku mshambuliaji wa chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) Yamiko Malile kushoto akiwania mpira huo wakati wa mashindano ya 36 ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimuya juu mchanganyiko Tanzania (SHIMIVUTA)

Mlindamlango wa timu ya soka ya chuo cha uhasibu Tanzania (TIA), Hemed Nassoro akiondoa hatari iliyoelekezwa langoni mwake dhid ya chuo cha walimu Nyerere Kivukoni (MNMA) wakati wa mashindano ya 36 ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimuya juu mchanganyiko Tanzania (SHIMIVUTA) katika uwanja wa jamhuri ambapo katika mchezo huo TIA ilishinda kwa bao 1-0.

MICHUANO ya 36 ya shirikisho la michezo ya vyuo vya elimuya juu mchanganyiko Tanzania (SHIMIVUTA) yanafikia tamati leo desemba 18 mwaka2011 kwa michezo miwili tofauti ya fainali ya itayofanyika kwenye uwanja wajamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza na mwanishi wa BLOGU HII kwenye uwanjawa jamhuri Morogoro Katibu Mkuu wa shirikisho hilo la SHIMIVUTA, AugustineMatem alisema kuwa mashindano hayo yanafikiatamati leo kwa michezo miwili tofauti ya fainali ikiwemo mchezo wa soka nanetiboli.

Matem alisema kuwa kwa upande wa mchezo wa soka timu nne zitapambana leo des 17 kwa ajili ya kucheza nusu fainali lengo ikiwa ni kupata timu mbili ambazo zicheza fainali kesho des 18 ambapo timu ambazo zimefanikiwa kucheza nusu fainali ni chuo cha elimu ya biashara (CBE) dhidi ya chuo cha uhasibuTanzania (IAA) wakati chuo cha serikaliza mitaa (LGTI) ikichuna na chuo cha uhasibu Tanzania (TIA) wakati katika fainaliya mchezo wa netiboli timu zilizotinga fainali ni chuo cha serikali za mitaa (LGTI)na chuo cha uhasibu Tanzania (IAA).

“leo kuna michezo miwili ya nusu fainali kwa upande wa soka ya kutafuta timu mbili zitazocheza fainali kesho na michezo ya kutafuta washindi wa tatu kwa michezo yote itafanyika leo pia lakini fainali ya michezo ya kikapu, wavu itafanyikaleo Bwalo la JKTZ wakati katika mbio za riadha washindi watapatana leo hii viwanja jamhurileo” alisema Matem.

Katika mchezo wa kikapu waliofanikiwa kuchezafainali ni chuo cha Mipango na maendeleo Vijijini (IRDP) na chuo cha elimu yabiashara (CBE) huku katika mchezo wa wavu timu zilizotinga fainali ni chuo chauhasibu Tanzania (TIA) dhidi ya chuo cha taasisi ya teknolojia Dar es Salaam (DIT),Alisema Matem.

Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa mashindano hayoyanatarajiwa kufungwa na mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro,Lidya Mbiaji ambaye atashuhudia michezo miwili ya fainali kwa mchezo wa soka nanetiboli na kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo zawadi za washindi wakwanza, wapili na watatu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: