Watu zaidi wauawa na dharuba nchini Ufilipino
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya vifo vilivyosababishwa na dhoruba kali nchini Ufilipino kwa sasa umefikia watu 976 huku wengine 46 hawajulikani walipo.
Wale nyumba zao ziliharibiwa wengine sasa wanaishi na familia pamoja na marafiki zao.
Karibu vituo 31 vya afya vimeharibiwa huku huduma za matibabu zikitatizwa na ukosefu wa maji.
Hata hivyo hakuna mkurupuko wowote wa magonjwa ulioripotiwa. Wale waliowapoteza wanzao au waliopoteza mali kwa sasa wanahitaji ushauri wa kisaikolojia.
0 comments:
Post a Comment