BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Wauzaji wa dawa za kulevya wanyongwa nchini Iran.


Watu watano wamenyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha na kuuza dawa za kulevya katika gereza moja kaskazini mwa mji wa Shahrud.

Taarifa kutoka shirika la habari nchini humo zimeeleza kuwa watu hao raia wa Iran ni wakazi wa miji mbalimbali ingawa taarifa zaidi kuhusu umri wao hazikuweza kutolewa.

Kwa mujibu wa takwimu za vyombo vya habari nchini humo, adhabu hii ya kunyongwa inafikisha idadi ya watu 277 walionyongwa nchini humo kwa mwaka huu pekee.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa watu 388 waliuwawa nchini humo mwaka 2010.

Kwa upande wa shirika la Amnest International limetaja nchi ya Iran kuwa ya pili kutekeleza adhabu ya kunyonga hadi kifo katika mwaka uliopita huku nchi ya China ikishika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo Iran imesema kuwa adhabu hiyo ni muhimu kwa ajili ya kulinda sheria na maagizo na kwamba hutumika baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: