TAWI la shirikisho la soka nchini TFF la Aspire mkoa wa Morogoro linatarajia kuwapatia mafunzo na mazoezi vijana zaidi ya 176 chini ya umri wa miaka 17 katika mchezo wa soka wenye lengo la kuibua vipaji ili kuviendeleza katika kituo cha soka nchini Kenya yanayoanza kesho uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Afisa Tawala Aspire tawi la Morogoro, Rajabu Kindagule alisema kuwa mafanzo hayo ikiwemo na mazoezi yatafanyika yatashirikisha zaidi ya vijana 176 ambapo yatafanyika kwa siku mbili huku vijana 10 wakitarajia kunufaika na mpango huo ambao wataenda nchini Kenya kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao ya soka.
Kindagule alisema kuwa mafunzo hayo na mazoezi mgeni rasmi atakuwa Profesa, Madundo Mtambo na yataanza kesho (leo) kwenye viwanja wa Moro Youth na Jamhuri chini ya Mkufunzi, John Simkoko na walimu wengine watatu wakiwemo Amri Ibrahim, Hussein Mau na Yahaya Belini ambao watakuwa na kazi ya kuangalia vijana hao na kuteua wataonyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka.
“Hii programu ipo chini ya TFF taifa ambapo Morogoro kuna tawi lake linalojulikana kwa Apire ambapo lengo kuu ni kuibua vipaji vya soka na kuviendeleza kwa vijana chini ya U17 katika mafunzo na mazoezi yetu tutachagua vijana 10 ambapo watakwenda moja kwa moja nchini Kenya kule wataungana na wenzao huko na watapata mafunzo mengine ya mchezo huo wa soka” alisema Kindagule.
Aidha Afisa Tawala huyo wa Aspire Morogoro alisema kuwa katika mafunzo hayo yataanza majira ya saa 8 hadi 12 jioni kwa siku ya leo jumamosi ambapo jumapili yataanza majira ya saa 2 asubuhi mpaka saa 6 mchana huku akiwataka vijana wenye uwezo wa kucheza soka kujitokeza katika mafunzo hayo na mazoezi kwani nafasi hiyo ni adimu kwao kwa mchezo wa soka.
0 comments:
Post a Comment