Raia wa Sudan Kusini wakabiliwa na njaa.
ZAIDI ya nusu ya raia wa Sudan Kusini wanakabiliwa na baa la njaa.
Shirika la chakula duniani limesema kuwa hali hiyo imechangiwa pakubwa na machafuko kati ya Sudan Kusini na jirani zao Sudan.
Katika taarifa ya shirika hilo limesema kuwa mapigano katika
maeneo ya mipaka na pia kufungwa kwa visima kadhaa vya mafuta kumetatiza
uchumi wa Sudan Kusini.
Ripoti inaonya kuwa kadiri machafuko
yanavyoendelea kati ya Sudan na Sudan Kusini ndivyo baa la njaa linazidi
kutatiza kwa wananchi wa Sudan Kusini.
Hapo awali ilikadiriwa kuwa watu takriban milioni 4.7 walikuwa wanakabiliwa na njaa lakini hivi sasa inaonekana hali ni mbaya zaidi.
Nchi hiyo kwa wakati huu inahitaji nafaka tani nusu milioni ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa wananchi wake.
Barabara mbovu zinafanya mambo kuwa magumu zaidi kwani usambazaji wa vyakula huwa vigumu zaidi kwa magari kupita kwa urahisi.
0 comments:
Post a Comment