Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga kulia akipeana mkono na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kikundi kata ya Kikundi Manispaa ya Morogoro, Donald Kulwa kushoto mara baada ya kupokea msaada wa madawati 30 yenye thamani ya sh1.8Mil kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza ambao walikuwa wakikaa chini wakati wa masomo yao kwa muda mrefu mkoani hapo, katikati ni Afisa Mwendeshaji wa mfuko huo Paulina Msanga.
Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga akiwaangalia wanafunzi wakiandika moja ya masomo baada ya kukabidhi madawati hayo.
Naye Afisa Mwendeshaji wa mfuko huo, Paulina Msanga akiwan na wanafunzi wengine wakiandika somo hilo.
Hapa wanafunzi wengine wakiwa wako makini na kuandika huku wakiwa wamekalia dawati jipy baada ya mfuko wa pensheni wa PPF kanda ya mashariki na kati kutoa msaada wa madawati 30 yenye thamani ya sh1.8Mil katika shule hiyo ya msingi.
SHULE ya msingi Kikundi iliyopo kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro imekabidhiwa msaada wa madawati 30 yenye thamani ya sh1.8Mil kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza ambazo walikuwa wakikaa chini kwa muda mfefu na mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) huku shule hiyo ikikabiliwa na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada hali shuleni hapo.
Akizungumza wakati wa kupokea huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Donald Kulwa alisema kuwa kutokana na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada kukosekana ina ulazimu uongozi wa shule hiyo kuomba msaada mungine kwa taasisi hiyo ili waweze kuongeza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi shuleni hapo.
Kulwa alisema kuwa kwa sasa wanafunzi 20 inawalamu kutumia kitabu kimoja kila siku wakati wa masomo yao ya kila siku na kuongeza kuwa msaada huo wa madawati hayo umesaidia kuwaondolea kero kwa wanafaunzi wa darasa la kwanza ambao walikuwa wakikaa chini kwa muda mrefu.
“Awali tulikuwa tunapata ruzuku kwa MEM wa vifaa mbalimbali kwa shule za msingi lakini baada ya kumaliza mktaba wao na serikali tunahangaika kupata mahitaji muhimu kama kukosa pesa za ukarabati wa vyumba vya madarasa, nunuzi wa vifaa vya kufundishia, kukosa pesa za kuandaa mitihani ya kila mwezi na matumizi mengine” alisema Kulwa.
Mkuu huyu alisema kuwa kukoseka kwa pesa kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa shule hiyo kunachangia mwanafunzi kushindwa kuelewa masomo yao na kudidimiza vipaji vyao vya taaluma kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo.
Naye Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni wa PPF kanda ya mashariki na kati, Astronaut Liganga alisema kuwa madawati hayo ni yametokana na mfuko huo kuwa na fao la elimu kwa ajili ya kuziwezesha shule za msingi na sekondari kupata vifaa mbalimbali vya elimu.
Liganga alisema kuwa mfuko huo wa PPF ndiyo pekee unaotoa fao hilo la elimu ukilinganisha na mifuko mingine ya kijamii ambapo imefanikiwa kupunguza baadhi ya matatizo katika shule ambapo Manispaa ya Morogoro tayari wamenufaika na mpanga huo.
0 comments:
Post a Comment