Rais wa Mpito wa Mali, Dioncounda Traore.
WAKUU wa serikali nchini Mali wamesema kuwa Rais wa Mpito, Dioncounda
Traore, amepelekwa eneo salama baada ya kupigwa hadi kuzirai na mamia ya
waandamanaji nchini humo.
Mamia ya waandamanaji walimshambulia Rais Traoure wakipinga mkataba
ulioafikiwa na Tume ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS,
ambapo Traoure ataendelea kutawala kwa hadi mwaka mmoja badala ya siku
40 pekee zilizokubaliwa miezi miwili iliyopita.
Mwandishi
wa BBC amesema kuwa shambulio hilo litawashtua wanadiplomasia waliokuwa
wakifanya kila juhudi kurejesha amani na utangamano nchini humo.
Muda wa kuongoza aliopewa kiongozi huyo, Djouncounda Traore ulitarajiwa kukamilika Jumatatu.
Lakini viongozi wa nchin za Magharibi mwa
Afrika, waliafikia mkataba na kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou
Sanogo kwamba BwTraore asalie mamlakani ili aweze kuongoza harakati za
uchaguzi na kumaliza harakati za waasi wa Tuareg.
Mkataba huo pia ulijumuisha mpango wa kukubalia
Sanogo atajwe kama kiongozi wa zamani alipwe mshahara wa rais na apewe
nyumba ya kifahari.
Mapinduzi hayo pamoja na harakati za waasi kuteka Kaskazini mwa Mali, yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao.
Mashirika ya misaada wanasema wana wasiwasi
mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Mali nchi ambayo pia inakumbwa
na baa la njaa.
Mwandishi wa BBC mjini Bamako, Martin Vogl
amesema kuwa wanajeshi waliwaruhusu baadhi ya waandamanji kuingia katika
ikulu ya rais ingawa bwana Traore hakuwepo wakati huo.
0 comments:
Post a Comment