MKUU wa mkoa wa
Morogoro, Joel Bendera anatarajia kuwaapisha wakuu wa wilaya nne za mkoa huo kufuatia
uteuzi mpya uliotangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivi karibu katika hafla
fupi ambayo itafanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo ya Morogoro.
Akizungumza na gazeti la
Mwananchi mjini hapa, Katibu Tawala mkoa wa Morogoro Eria Ntandu alisema kuwa kuapishwa
kwa wakuu hao wapya wa wilaya zitawapafursa ya kuanza kazi mara moja baada ya
kuchukua nafasi za watangulizi wao wengine waliopandishwa madaraja na wengine
kubadilishwa vituo vya kazi.
Aliwataja wakuu hao wa
wilaya na vituo vyao vipya ambao wanatarajia kuapishwa na mkuu huyo wa Mkoa
kuwa ni pamoja na Saidi Amanzi – Morogoro, Elias Tarimo – Kilosa, Hassan Masala – Kilombero, Antony Mtaka – Mvomero wakati Fransic Miti ataendelea kubakia kituo
chake cha kazi cha wilaya ya Ulanga.
Ntandu alisema uteuzi
huo utafanya wilaya nne za mkoa wa Morogoro ziliachwa wazi kwa kipindi kirefu
baada ya wakuu wa wilaya hizo kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa akiwemo, Saidi Thabiti
Mwambungu aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mikoa ya Ruvuma akitokea wilaya ya Morogoro.
Wengine ni Fatma Mwassa
aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora akitokea wilaya Mvomero na Mhandisi Ernest
Ndikolo kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza akitokea wilaya ya Kilombero.
Alisema kuwa kabla ya
kuteuliwa kwa wakuu hao wapya wa Wilaya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kilosa Halima
Dendego alikuwa akikaimu wilaya za Mvomero,Morogoro na Francis Mitti alikuwa
akikaimu wilaya ya Kilombero kutokana na wilaya hizo kukosa viongozi kwa
kipindi hicho ambapo hata hivyo naye Halima Dendego ameteuliwa kuwa mkuu wa
wilaya ya Tanga Mjini.
Katibu Tawala
huyo alisema kuwa sherehe hizo zinatarajiwa kuanza majira ya saa 5 mei 17 asubuhi
na kumalizika majira ya saa 6:30 mchana ambapo zitafanyika katika viwanja vya
Ikulu ndogo ya Mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment