BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBIO ZA MAGARI ZA LARRY HORN MOTO CROSS 2012.



Dereva chipukizi wa mbio za magari kutoka klabu ya Mt Uluguru Motor Morogoro, Kartic Valambia na msaidizi wake Saidi Bondi wakiwa katika mazoezi kwa ajili ya kusiriki mashindano ya magari ya Larry Horn Moto Cross 2012 yanayotarajia kufanyika agosti 4 na 5 mwaka huu nje kidogo ya Manispaa hiyo katika eneo la Mkundi mkoani hapa.


DEREVA chipukizi wa mbio za magari kutoka katika timu ya Mt Uluguru Motor, Kartic Valambia (31) amesema kuwa mazoezi makali anayofanya ana imani ya kushika nafasi ya kwanza wakati wa mashindano ya magari ya Larry Horn Moto Cross 2012 yatayotarajiwa kufanyika agosti 4 na 5 mwaka huu eneo la Mkundi Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mazoezi katika eneo hilo la Mkundi, Valambia alisema kuwa mikakati aliyoweka hivi sasa ni kufanya mazoezi kwa umakini ili kuweza kumudu kuzitambua kona na kumaliza muda uliopangwa na kutwaa nafasi ya kwanza.

Valambia alisema anafahamu kuwa mashindano hayo yatakuwa na upinzani mkali lakini hilo amejipanga ili kukabiliana na changamoto hizo licha ya kuwa mashindano hayo ni mara yake ya kwanza kushiriki.

“nina imani kubwa sana kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya mbio za magari haya ya Larry Horn Moto Cross 2012 na hivi sasa ninachomba ni gari langu liwe katika hali mzuri na sina hofu sana na wapinzani wangu hata kidogo licha ya kuwa ni mara yangu ya kwanza kushiriki mashindano ya magari nitafanya kwani haya mazoezi ninayofanya yananipa matumaini ya kuwa mshindi” alisema Valambia.

Naye Mwenyekiti wa klabu ya Mt Uluguru Motor Morogoro, Pankaj Valambia alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo ya Larry Horn Moto Cross 2012 yameanza kwa baadhi ya washiriki kuanza kufanya mazoezi kwa madereva wa mbio za magari, Kartic Valambia (31) na Evans Harras wakati upande wa mbio za pikipiki wakiwa na idadi ya nane.

Valambia alisema kuwa mbio hizo zitakuwa za kilometa moja na mojawapo ya sifa za mshiriki kushirki katika mashindano hayo kwanza lazima awe mwanachama wa klabu ya Mt Uluguru Motor Morogoro na washiriki wengine wanakaribishwa kutoka katika klabu za michezo ya mbio za magari na pikipiki kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na mikoa mingine.

Katika siku ya kwanza dereva, Kartic Valambia akitumia gari aina ya Isuzu Piazza aliweza kutumia muda wa dakika 2:55:15 katika umbli huo wa kilometa moja huku Evans Harras alitumia kwa dakia 2:07:26 kwa gari aina ya Land Rover 110 wakati wa mazoezi hayo na kuwa muda huo unaweza kupungua endapo washariki wataweza kuingia na magari mazuri zaidi tofauti na hayo yaliyotumia muda huo. Alisema Mwenyekiti huyu.

Kwa upande wa mbio za magari ambao washiriki wamenza kujitokeza ni madereva wawili huku pikipiki wakiwa nane na kuwa idadi kubwa ya washiriki watarajiwa kujitokeza wiki moja kabla ya mashindano hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: