Rais mpya wa Misri, Morsi.
EGYPT.
Mgombea wa Muslim Brotherhood, Mohamed Morsi ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa duru ya pili ya urais nchini Misri.
Umati mkubwa ulikuwa ukishangilia kwenye eneo la Tahrir Square ambako wafuasi wa mgombea Morsi walikusanyika hivi juni 24 mwaka huu.
Sherehe za umati huo zilikuwa tofauti baada na karibu mwaka mmoja na nusu uliopita wakati wananchi wa Misri walipojazana katika eneo hilo wakati wa maandamano ambayo yaliiangusha serikali ya rais, Hosni Mubarak.
Tume ya uchaguzi ya Misri ilitakiwa itoe matokeo wiki iliyopita lakini ilisema itahitaji muda zaidi kuchunguza tuhuma za ubadhirifu ambazo wagombea wote wawili waliwasilisha.
Kabla ya kutolewa kwa tangazo la matokeo ya kura maafisa walipeleka majeshi zaidi kwa ajili ya usalama katika mitaa mbalimbali ya mji wa Cairo na kwenye taasisi muhimu za serikali.
Hadi sasa hakuna ghasia zozote ambazo zimeripotiwa.
0 comments:
Post a Comment