JUMLA ya sh15Mil zinatarajia kutumika katika ukarabati ya uwanja wa jamhuri kwa ajili ya kutumika katika michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa mwaka 2012/2013 na ile ya mashindano ya shirikisho la Michezo ya Idara za Serikali, Wizara na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) mwanzoni Agosti mwaka huu mkoani hapa.
Sehemu ambazo zinatarajiwa kukarabatiwa ni pamoja na eneo la kuchezea mpira wa miguu, netioboli, vyoo, sehemu ya kukimbilia wanariadha na sehemu ngingine na kuwa moja ya sababu kubwa iliyochangia uwanja huo kushindwa kukarabati ni ghalama kubwa za uendeshaji.
Akizungumza na gazeti hili Meneja wa uwanja wa jamhuri Morogoro katika mahojiano maalum, Herman Ndisa alisema kuwa kuna fedha kiasi cha sh15Mil zinatarajiwa kupatikana na kazi kubwa ya fedha hizo zitatumika moja kwa moja katika kukarabati uwanja huo.
Ndisa alisema kuwa kiasi cha sh10Mil zitatolewa kwa mmoja wa wafadhili wa klabu ya Polisi Morogoro SC ambayo itatumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani na kiasi cha sh5 kitatolewa na shirikisho la Michezo ya Idara za Serikali, Wizara na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) kwa ajili matumizi ya mashindano hayo mwaka huu yatayofanyika mkoani hapa.
“Tunatarajia kupata fedha kiasi cha sh15Mil mwezi huu ambazo zitatoka kutoka kwa wadau wetu wawili kati ya hao ni mmoja wa wafadhili wa klabu ya Polisi Morogoro SC ambaye atatumia fedha hizo kukarabati uwanja huo na
Kiasi cha sh5Mil tunatarajia kupata kutoka kwa SHIMIWI ambazo nazo zitutaelekeza katika ukarabati huo” alisema Ndisa.
Ndisa alisema uwanja huo haujakarabatiwa kwa muda mrefu kutokana na uongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Morogoro kushindwa kukarabati hivyo mara baada ya kupata fedha hizo zitaelekezwa moja kwa moja katika ukarabati huo ambapo utapunguza baadhi ya kero ndani ya uwanja huo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / SH15MIL KUTUMIKA KUKARABATI UWANJA WA JAMHURI KWA AJILI YA MICHEZO YA LIGI KUU YA VODACOM MSIMU WA MWAKA 2012/2013 NA SHIMIWI MOROGORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment