Mshambuliaji
wa timu ya soka ya wilaya ya Ulanga Saidi Matumla (katikati) akitafuta
mbinu ya kuwatoka walinzi wa wilaya ya Kilosa, Bahati Emmanuel kushoto na
Bonifance Jonathan kulia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA)
ngazi ya mkoa wa Morogoro yaliyoanza kutimua vumbi na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika uwanja wa
jamhuri mjini hapa.
TIMU
ya
soka ya wilaya ya Ulanga imeitandika wilaya ya Kilosa kwenye mchezo
mkali na kusisimu wakati wa mchezo wa ufunguzi mashindano ya umoja wa
michezo kwa shule za msingi na taaluma Tanzania (UMITASHUMTA)
ngazi ya mkoa wa Morogoro yaliyoanza kutimua vumbi kwa bao 2-1 katika
uwanja wa
jamhuri mjini hapa.
mashindano hayo ambayo yanashirikisha wanamichezo kutoka wilaya sita za mkoa wa Morogoro ikiwemo Morogoro Vijijini, Mvomero, Kilosa, Ulanga, Kilombero na Morogoro yatadumu kwa siku tatu lengo likiwa kusaka vipaji vya michezo mbalimbali ili kuweza kushiriki mashindano ya Umitashumta ngazi ya Kanda Kibaha mkoani Pwani.
Katika mchezo huo Ulanga ndiyo walianza kutawala mchezo huo na kujipatia bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Adolph Machege baada ya kupokea pasi ya Mahamdu Chambwane na kujaza mpira huo kimiani huku bao la pili likipatikana katika dakika ya 24 lililofungwa na Shaffi Balikia kwa mkwaju wa penalti baada ya mlinzi wa Kilosa kufanya makosa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Shaaban Juma kutoa adhabu hiyo.
Kilosa walijipatia bao la kufutia machozi Kalama Iddi aliyefungwa kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo na kuwazidi ujanja walinzi wa Ulanga na kupachika bao hilo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Ulanga kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Katika mchezo wa netiboli wilaya ya Kilosa iliweza kuifunga wenzao wa wilaya ya Mvomero katika mchezo mkali na kusimumua mbao Kilosa walishinda kwa vikau 9-5.
Mfungaji Levinota
Mabruki ndiye aliyeiwezesha Kiloosa kuibuka na ushindi huo kwa kufunga vikapu
vyote tisa wakati vikapu vya Mvomero vilifungwa na wafungaji Halima Omari
aliyefunga tano na Saumu Juma akifunga manne.
Michezo hiyo inaendelea kwa timu za Manispaa zikicheza na wilaya ya Mvomero katika muendelezo wa michezo hiyo.
0 comments:
Post a Comment