Fuvu za vichwa vya Wanyarwanda waliouawa mwaka wa 1994.
Katika mahakama hiyo ya kimataifa kwa ajili ya nchini ya Rwanda ilisema kuwa waziri huyo wa zamani alichochea mauaji ya watu kati ya 15 hadi 60 wa kabila la Tutsi mwezi Aprili mwaka wa 1994 katika eneo la Nyabikenke.
Hukumu hiyo pia ilisema kuwa Nzabonimana alichochea watu mara tatu hadharani mwezi huo kuwauwa Watutsi na akaingia kwenye makubaliano ya kuwauawa watu wa kabila hilo na serikali ya muda ya Rwanda wakati huo.
Nzabonimana alikuwa waziri wa maswala ya vijana wa Rwanda katika serikali ya muda iliyoundwa mwaka wa 1994.
Alikamatwa mwezi Februari nchini Tanzania na kukabidhiwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Rwanda yenye makao yake mjini Arusha, Tanzania.
Wanamgambo wa Kihutu inakisiwa waliuawa watu laki 8 wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri wakati wa mauaji ya halaiki mwaka huo wa 1994.
Mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilibuniwa kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi ya wahusika wakuu wa mauaji ya halaiki ya nchini Rwanda.
0 comments:
Post a Comment