Mmoja wa ng'ombe akiwa kwenye Fuso huku chini ya jicho lake ikiwa na jeraha inayodaiwa kuwa ni yarisasi aliyopigwa na askari wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Mikumi mkoani Morogoro juni 27 mwaka 2012 katika eneo la mpaka wa kati ya hifadhi hiyo na kijiji cha Ngaite-Luhoza kata ya Tindka wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na ng'ombe 17 walipigwa risasi huku watano wakipoteza maisha mkoani hapa.
Mfugaji wa jamii ya kimasai katika kijiji cha Ngaite-Lohoza kata ya Tindika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Ibrahim Oloishuro
wa pili kutoka kulia akiangalia waendesha pikipiki maarufu bodaboda
wakiwa wamepakia nyama ya ng'ombe ambao wanadaiwa kupigwa risasi na
askari wa hifadhi ya taifa ya wanyama pori ya Mikumi katika eneo
linalodaiwa kuwa ni mpaka wa hifadhi hiyo na kijiji cha Ngaite-Lohoza
kwa madai ya kuingia ndani ya hifadhi ambapo jumla ya ng'ombe 17 wa
mfugaji huyo walidaiwa kulipigwa risasi na watano walikufa huku wengine
wakijeruhiwa mkoani hapa.
Bodaboda wkiwa na viroba nyenye nyama ya g'ombe hao wakielekea katika kijiji cha Doma kwa ajili ya kuuza baada ya kununua kwa bei nafuu.
Mfugaji wa kijiji cha Ngaite-Luhoza, Ibrahim Oloishuro akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuwasafirisha ng'ombe wanane ambao wwanadaiwa kupigwa risasi na askari wa hifadhi ya Mikumi na kujeruhiwa muda mfupi kabla ya kuondoka katika eneo la kijiji hicho kwa ajili ya kuwapeleka mjini ili akawauze kwa bei ya hasara.
ASKARI wa hifadhi ya taifa ya Mikumi iliyopo Mkoani
Morogoro wanatuhumiwa kuwaua zaidi ya ngombe 11 mali ya mfugaji wa jamii ya
kimasai wa kijiji cha Ngaite Luhoza kilichopo kata ya Tindika Wilaya ya Kilosa kwa
kuwapiga risasi na kuwasababishia hasara ya mamilioni ya fedha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika
kijiji cha Ngaite-Luhoza mfugaji, Ibrahim Oloishuro alisema kuwa kwa nyati tofauti
amepoteza madume ya ng’ombe 11 baada ya kudaiwa kufa baada ya kupigwa risasi na
askari wa hifadhi hiyo juni 12 na juni 27 mwaka huu na kusababisha hasara kwa mfugaji
huyo mkoani hapa.
Oloishuro alisema kuwa hasara hiyo ameipata baada ya
ng’ombe sita kufa katika tukio lililotokea juni 12 kufuati askari kuwapiga
risasi wakati tukio la pili lilikuwa kubwa zaidi ambalo jumla ya ng’ombe 17 kupigwa
risasi na askari hao wakati wakiwa wanakunywa maji katika mto Luhosa ambao
unatengenisha kijiji hicho cha Ngaite-Luhosa na hifadhi ya Mikumi.
“Hapa kuna tatizo kubwa sana kati ya wafugaji wa jamii
ya kimasai katika kitongoji cha Luhoza na hao jirani zetu wa hifadhi lakini
wameanzisha tabia ya kuwapiga risasi mifugi hasa madume sasa sijajua lengo lao
nini kwa kuchagua kupiga madumu na wengi wao wamekuwa wakipoteza maisha baada
ya kupigwa ama wengi siku tatu baadaye” alisema Oloishuro.
Oloishuro alisema kuwa ng’ombe wanaolengwa zaidi kwa
kupigwa risasi ni wale madume na kuongeza kuwa tukio la juni 27 lilitokea
majira ya saa 10 jioni katika mto huo madume 16 ndiyo yaliyopigwa risasi kati
yao watatu walikufa katika eneo la tukio na wawili walikufa njiani wakati
wakirudi nyumbani wakiwemo na wengine waliojeruhiwa vibaya walijikongoja hadi
katika zizi huku sehemu mbalimbali za miili yao zikiwa zimetapakaa damu.
“Wale vijana wangu wanachunga ng’ombe wangu baada ya
kusikia miilio ya risasi walikimbia na kurudi nyumbani na kuwaacha ng’ombe
katika eneo la mpaka ule wa mto Luhoza na tulipoenda katika eneo la tukio
tulikutana na baadhi ya ng’ombe wakirudi nyumbani na wawili walikufa njiani
wakati watatu tuliwaona eneo la mto nimepata sana hasara sijui nini fanye nini
mimi” alisema Oloishuro.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Ngaite Luhoza kata ya
Tindika Wilaya ya Kilosa, Matinda Koilekeni alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na sio tukio la kwanza kutokea katika kitongoji hicho Luhoza bali kimekuwa
kikitokea mara kwa mara na wafugaji katika kitongoji hicho kinachokaliwa na
wafugaji ndiyo wameathiriwa kwa kiwango kikubwa na matukio ya namna hiyo.
Koilekeni alisema kuwa matukio ya kupigwa ng’ombe
risasi hayakutokea kwa wafugaji wa kitongoji cha Luhoza pekee yake bali hata na
wale wafugaji wavamizi wa sehemu nyingine nao ng’ombe wao wameuawa kwa kupigwa
risasi na askari wa hifadhi hiyo kwa nyakati tofauti.
“kwa mifugo iliyopigwa risasi na kufa ni mingi sana
lakini kwa upande wangu baada ya kupata malalamiko yao hawa wafugaji ya kupigwa
risasi na askari wa hifadhi nilifanya mawasiliano na viongozi wa juu wa hifadhi
lakini majibu waliyonipa hayakuniridhisha hivyo baadhi ya wafugaji waliamua
kwenda kwa bungeni kwa lengo la kuonana na waziri wenye dhamana ili kupeleka
kilio chao hicho cha mifugo yao kupigwa risasi” alisema Koilekeni.
Obeid Kipilingai Kalaita (34) mfugaji ambaye naye
alikumbwa na tukio la kupoteza ng’ombe mwaka 2010 alisema kuwa yeye amewahi
kupoteza ng’ombe 357 lililotokana na askari wa hifadhi hiyo kuteka mfugaji mia
nane wanaodaiwa kuingia ndani ya hifadhi
na kukaa chini ya ulinzi wao kwa siku saba bila kupewa chakula.
Kalaita alisema kuwa baada ya kufuatia ng’ombea hao
ni ng’ombe 357 ndiyo aliofanikiwa kuwapata na wengine haieleweki wamenda wapi
na kueleza kuwa dhana ya ujirani mwema haizingatiwi kwa askari hao kwani wamekuwa
wakiwapatia hasara na kudidimiza maendeleo ya mifugo.
Alisema kuwa ukiachilia mbali kwa yeye kupoteza ng’ombe
357 mwaka 2010 kuna baadhi ya wafugaji wengine nao wamepata hasara kwa koteza
mifugo yao iliyotokana na sababu mbalimbali kufuatia askari kudaiwa kupigwa
risasi ama kuwapora nje ya mipaka ya hifadhi.
Kalaita aliwataja wafugaji hao ambao mifugo yao
imekufa na kuwasababishia hasara kubwa kuwa ni Robina Niuyai ng’ombe 30, Kafuna
Steti ng’ombe saba, Kiunja Coaster ng’ombe watano, Msando Parokore ng’ombe
watano wa kitongoji cha Luhoza kata ya Tindika.
Wengine ni Mataiyani Simanga kwa kupoteza amepoteza
ng’ombe saba, Lowassa Niuyai ng’ombe nane wakiwa wafugaji wa kijiji cha Kiduhi
katika wilaya hiyo ya Kilosa.
Kutokona na hasara wanayopata wafugaji hao wanaiomba
serikali kuu kuangalia upya sheria za mifugo kuingia ndani ya hifadhi kwani
itasaidia kuondoa hasara isiyo ya razima kwa wafugaji na kushauri kufuata
utaratibu unaotumiwa na hifadhi za Ngorongoro ambapo mifugo imekuwa ikilisha ndani
ya hifadhi tofauti na hifadhi ya Mikumi wakati mungine imekuwa ikiingia bila
kukusudia.
Hata hivyo juhudi za kumtafuta mkuu wa hifadhi ya
taifa ya Mikumi mkoani Morogoro hazikuweza kufanikiwa kutokana na namba yake ya
simu ya kiganjani kutopatikana.
0 comments:
Post a Comment