Na Jabir Idrissa.
NAIBU Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS), Jack Zoka ametajwa kuwa miongoni mwa wanaopanga mkakati wa kuangamiza wanaodaiwa kuikosoa serikali, MwanaHALISI limeelezwa.
Aidha, ametajwa kuwa mmoja wa waliounda mpango wa kutekwa na kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka ambaye hivi sasa anaendelea na matibabu Afrika Kusini.
Taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka vyanzo mbalimbali zinasema, Zoka ni mtuhumiwa Na. 1 katika utekelezaji wa mpango wa siri wa mauaji, utekaji na utesaji ambao umeandaliwa mahususi na kwa watu maalum.
Miongoni mwa wanaotajwa kutaka kuangamizwa, ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibord Slaa, mbunge wa Ubungo kupitia chama hicho, John Mnyika na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea.
Bali Zoka hakupatikana juzi Jumatatu kutoa kauli yake juu ya tuhuma hizi.
Mwandishi alimwita Zoka tangu saa nane mchana hadi saa 12.55; lakini simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilijibu kuwa mwenye namba hiyo hapatikani.
Hatimaye mwandishi alipeleka ujumbe kwa Zoka uliosema: “Natumai umzima wa afya. Mimi mhariri wa MwanaHALISI nataka uzungumzie tuhuma za viongozi wakuu wa Chadema, kuwa TISS na wewe binafsi, mmepanga kuua baadhi yao. Unasemaje?”
Zoka aliombwa pia kutoa kauli juu ya taarifa katika mitandao, zinazomtaja yeye binafsi kuwa nyuma ya mpango uliofanikisha kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.
Dk. Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini 30 Juni, kwa michango ya madaktari wenzake, watu mbalimbali na kile kilichoelezwa kuwa “msaada mkubwa wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Dk. Reginald Mengi.”
Kwa mujibu wa mawasiliano ya imeili yaliyotumwa na mmoja wa watoa taarifa wa ndani wa Dk. Slaa na Mnyika, mpango wa kuwateketeza watu hao umeandaliwa mahususi ili “kuwatisha katika harakati za kutetea wananchi wanyonge.”
Mtoa taarifa huyo kutoka ndani ya idara ya usalama ameeleza, katika mawasiliano yake ya 27 Juni 2012, kuwa kuna mpango wa kuteketeza maisha ya Dk. Slaa na Mnyika; na kwamba mpango huo unaratibiwa moja kwa moja na Zoka.
“…the information I'm giving you is authentic (taarifa ninazokupa ni sahihi na makini). Tayari kuna timu imetumwa kwenda Dodoma kufuatilia mienendo ya Mnyika kwa maana ya mahali alipofikia, mahali anapopendelea kutembea na kula chakula na marafiki anaokuwa nao mara kwa mara, hasa wanawake kama wapo,” anaeleza mtoa taarifa.
Anasema, “Hii timu inafanya kazi moja kwa moja kwa maelekezo ya Zoka na wamepewa kazi ya kutathmini njia bora ya kumdhuru Mnyika bila kuacha trace (unyayo) yoyote. Katika options (njia za kutumia), kuna kuweka sumu kwenye maji, chakula au (kumpiga) sindano. Kuna matumizi ya ajali au ujambazi.”
Andishi hilo linasema, “Katika ajali, timu hiyo imeelekezwa kuangalia mbinu kama waliyowahi kuijaribu kwa Mwakyembe (Dk. Harrison Mwakyembe mbunge wa Kyela CCM). Hapa kuna vijana wamefundishwa kikamilifu njia hii. Mafunzo yao yaliandaliwa (jina la nchi tunalo) mwishoni mwa mwaka jana.”...
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MWANAHALISI LANUNULIWA KAMA KARANGA KUTOKANA NA HABARI YA KUDAIWA KUFICHULIWA KWA NJAMA ZA KUWAUA KUBENEA, DK SLAA, MNYIKA NA DK ULIMBOKA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment