MARCUS AGIUS.
Marcus Agius aliamua binafsi kujiuzulu kutokana kwa
kile alichotaja katika taarifa yake ya kujiuzulu kama pigo kubwa
linalotokana na kuharibiwa sifa kwa kampuni hiyo kwa sababu ya madai ya
kuwalaghai wateja kupitia nyongeza haramu ya riba.
Wito umetolewa kuwa afisa mkuu mwandamizi wa
kampuni hiyo Bob Diamond ajiuzulu kwa sababu alikuwa akisimamia
uwekezaji wa benki hiyo wakati mpango ulipofanywa kulaghai wateja
kupitia kwa riba inayotozwa katika benki hiyo.
Hata hivyo wakurugenzi wa Barclays wameamua kuwa Diamond ataendelea kufanya kazi.
Kwa hivyo Agius ambaye pia ni mwanachama
wa Bodi aliamua huku akiungwa mkono na wenzake kujitwika lawama zote
zinazotokana na madhambi yanayokabili Benki ya Barclays na hasira yote
waliyo nayo wenye hisa wa benki hiyo.
Mtu anayetazamiwa kuchukua mahali pake ni
mkurugenzi mwingine, Sir Mike Rake ambaye kwa sasa atalazimika
kujiuzulu vyeo vyake vya kuwa mwenyekiti wa Easyjet na BT.
Naye Diamond hajajiondoa katika lawama
bado kwani atahojiwa na Wabunge kuhusu mawasiliano ya siri ya mwaka wa
2008 kati yake na naibu wa Gavana wa Benki Kuu, Paul Tucker.
Meneja wa Barclays wanaamini kuwa ni katika
mawasiliano hayo ambapo Benki Kuu ya Uingereza iliamuru Benki hiyo
kudanganya kuhusiana na riba inayotozwa.
Hiyo haikuwa kweli lakini Bwana Diamond
atalazimika kuwaeleza Wabunge anachokumbuka Bwana Tucker akimweleza
wakati ule na kile ambacho baadaye aliwaeleza wafanyakazi wenzake.
Itakuwa aibu kubwa kwao iwapo yeye au Bwana Tucker watagunguliwa kwamba waliwashawishi wenzao kulaghai kupitia riba haramu.
0 comments:
Post a Comment