BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA YASHUTUMIWA KURUHUSU MELI ZA IRAN KUTUMIA BENDERA YAKE.

INADAIWA KUWA IRANI INATUMIA BENDERA YA TANZANIA KATIKA MELI ZAKE KUEPUKA VIKWAZO VILIVYOWEKWA NA MAREKANI NA UMOJA WA ULAYA.
Meli za mafuta za Iran zikiwa safarini

TANZANIA imetakiwa kusimamisha matumizi ya bendera yake katika meli za mafuta za Iran ikiwa kama juhudi za nchi hiyo kukwepa vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Mbunge mwandamizi katika baraza la wawakilishi la bunge la Marekani, Howard Berman mdemokrat kutoka California amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kumtaka asimamishe matumizi ya bendera ya Tanzania katika meli za Iran baada ya ripoti kuwa meli za kampuni ya usafirishaji mafuta ya Iran NITC zimesajiliwa kama meli za Tanzania na kupeperusha bendera ya nchi hiyo.

Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar Issa Haji Gavu amesema katika mahojiano na Sauti ya Amerika VOA kuwa meli hizo zilisajiliwa Zanzibar kama meli za Uingereza na sio meli za Iran kama inavyodaiwa.

"Maombi yaliyowasilishwa katika usajili yalisema meli hizo ni za Uingereza sio kama meli za Iran" alisema Haji Issa Gavu, Naibu Waziri Zanzibar.

Mbunge Berman alisema katika barua hiyo ya Juni 29 kuwa misaada ya Marekani kwa Tanzania itakuwa hatarini endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Katika barua hiyo Berman alisema kuwa "inasikitisha sana kuona kuwa serikali yako imechukua hatua zinazokiuka ushirika wa kimataifa unaoshirikiana kwa njia za amani ikiwa ni pamoja na vikwazo vya uchumi kubadili mwenendo hatari wa serikali ya Iran.

Uamuzi wa kuruhusu NITC kutumia bendera ya Tanzania unatilia mashaka sifa za Tanzania kimataifa.

Tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka saba iliyopita Tanzania imekuwa ikipata misaada mikubwa kutoka Marekani katika mpango wa afya wa PEPFAR ulioanzishwa na Rais George Bush na mpango wa Millenium Challenge unaoshirikiana na nchi zinazoonyesha maendeleo duniani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: