Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Bombom ya Dar es Salaam Ismail Chuji kushoto akimtoka mlinizi wa Young Boys ya Chamwino Morogoro, Richard Chiwalanga kulia wakati wa mashindano yanayoendelea ya Winome Cup 2012 katika uwanja wa Sabasaba mjini hapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Bobom kupata ushindi wa bao 7-0.
TIMU ya soka ya vijana ya Bombom ya jijini Dar es Salaam chini ya umri wa miaka 15 imeendeleza ubabe katika mashindano ya Winome Cup 2012 chini ya umri huo baada ya kuibuka na ushindi mnono katika michezo miwili mashindano ambayo yameanza kutimua vumbi julai 9 mwaka huu kwenye viwanja vinne tofauti mkoani hapa.
Katika mchezo wao wa kwanza vijana hao wa Bombom walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Afrikan City katika uwanja wa Moro Youth wakati mchezo wa pili wakiongeza idadi ya mabao ya 7-0 kwa kuifunga Young Boys Kids ya Chamwino Morogoro mchezo uliochezwa uwanja wa Sabasaba.
Wakati timu ya Tesa ya jijini Dar es Salaam nayo ilifuata nyayo hizo za kuendeleza wimbi la ushindi kwa wapinzani wake baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Kikundi waliowatandika bao 4-1 katika mchezo wa pili huku mchezo wa ufunguzi wakiilaza Mwere Kids ya Morogoro kwa kuikung’uta bao 2-0.
Mabaingwa watetezi wa kombe la mashindano hayo timu ya Villa Squard yenyewe ikikubali kichapo cha bao 2-0 dhidi ya vijana wa Anglikana Kids katika mchezo wao wa ufunguzi uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri.
Washambuliaji Rashid Kijembe aliweza kuifungia timu yake ya Bombom mabao mawili katika ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Afrikan City huku washambuluiji, Ayoub Pilo, Karim Athman, Haji Salum wakifunga bao moja moja kwenye mchezo huo.
Vijana hao wa Bombom waliendeleza ubabe kwa vijana wenzao wa Young Boys Kids kwa mshambuliaji wao tegemeo, Omari Mambeta kupachika mabao matatu pekee yake huku mshambuliaji, Ayoub Pilo akifunga mabao mawili wakati washambuliaji wengine wa timu hiyo, Rashid Kijembe na Ismail Chuji wakifunga bao moja moja katika mashindano hayo yanayoendelea mjini hapa.
Katika michezo mingine timu ya Kikund Kids ilikubali kipigo cha bao 3-2 dhidi ya Barcelona kids zote za Morogoro wakati Moro Kids ikiitandika Kurasini ya Dar es Salaam bao 2-1 na Al Futuh wakiizaba Eleven Killers bao 1-0.
Mratibu wa mashindano hayo ya Winome Cup 2012, Omari Mkesa alisema kuwa jumla ya timu 20 zinashiriki michezo ya mashindano hayo ambayo yanalengo la kuendeleza vipaji na kuibua huku timu14 zikitoka Manispaa ya Morogoro na moja ikitoka wilaya ya Mvomero wakati timu tano zikitoka katika jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment