Mkazi wa Kichangani, Yuster Manasa (40) akipalilia mahindi huku akiwa na mtoto mgongoni katika shamba lake lake kata ya Kinglwira Manispaa ya Morogoro lililolimwa kwa kilimo cha umwagiliaji ambapo leo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima nane nane nchini.
Balozi wa nchi ya Indonesia nchini Yusthranto Sungadio kulia akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tanseed International, Isaka Mashauri kushoto akifafanua jambo juu ya teknolojia ya mbegu ya mahindi ya chakula malisho (FOOD-FEED) wakati balozi huyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya wakulima kanda ya mashairiki uwanja wa Mwl Julius Nyerere Nane Nane yanayofikia kilele agosto 8 mkoani hapa, katikati ni kuu wa mkoa wa Tanga Chiku Gallawa.
Hapa Balozi huyo wa nchi ya Indonesia nchini Yusthranto Sungadio akiangalia zao la mtama katika vipando vya banda la Bagamayo mkoa wa Pwani katika maonyesho hayo.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakimwangalia Swala aliyekaushwa katika banda la hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Mikumi iliyopo katika mkoa wa Morogoro
Mamba wakiwa nje ya bwala lao katika banda la halmashauri ya wilaya ya Bagamayo
mkoa wa Pwani katika maonyesho hayo ambayo leo ni kilele chake.
0 comments:
Post a Comment