KLABU za Yanga na Mtibwa Sugar zimeingiza jumla ya sh38.3Mil katika pambano lao la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara katika mzunguko wa pili uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa Katibu Mtendaji wa chama cha soka Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema kuwa jumla ya sh38.3Mil zimepatikanana katika mchezo wa Yanga na Mtibwa Sugar kutokana na watazamaji 12, 677 ambao walijitokeza katika mchezo huo.
Katika mchezo huo ilishuhudia mashabiki wa Yanga wakiinamisha vichwa chini baada ya mchezo kumalizika baada ya klabu yao kukubali kipigo cha bao 3-0 katika mchezo mkali na kusisimua uliotawaliwa kwa kiasi kikubwa na Mtibwa Sugar katika ligi hiyo.
Semka alisema kuwa mgawanyo wa fedha hizo ziligawanywa katika makundi tisa tofauti kulingana na viwango vilivyowekwa ikiwemo klabu kupata mgao wa sh8,187, 730Mil huku kodi ya mapato (VAT) ikipata sh6,845, 580Mil wakati uwanja ukipata kiasi cha sh4,163,253Mil.
Alitaja ghalama za tiketi katika mchezo huo kuwa sh2,5354Mil, wakati ghalama za mchezo ni sh2,497,95Mil, kamati ya ligi ikipata mgao wa sh2,497,951Mil, mfuko wa maendeleo ya mpira (FDF) sh1,248,975Mil na chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) ikiambulia sh971,425.
Semka amewashukuru wapenzi na wadau wa soka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kwa kujitokeza kwa uwingi katika mchezo baina ya Mtibwa Suga na Yanga.
Aidha Semka amewaomba mashabiki hao kujitokeza kwa uwingi kama huo katika mchezo wa mzunguko wa tatu kati ya Polisi Moro SC dhidi ya Toto Afrika ya Mwanza unaotarajia kuchezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Septemba 26 mwaka huu katika mfululizo wa ligi hiyo.
WAKATI huo huo baada ya Yanga kupigwa bao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2012/2013 mashabiki wameibuka na kauli mbalimbali huku wakidai kuwa sehemu ya ulinzi ilifanya makosa mengi na kuchangia kupoteza mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri jana.
wakizngumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo mashabiki wa klabu hiyo mkoani hapa walisema kuwa moja ya sababu ya Yanga kutandikwa bao 3-0 zimetokana na safu ya ulinzi kufanya makosa mengi yaliyopelekea Mtibwa Sugar kuyatumia vizuri na kuibuka na ushindi huo mnono wa bao 3-0.
Mmoja wa mashabiki hao, Hassan Omari yeye aliilaumu safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya mlinzi wake ambaye ni nahodha, Nadir Haroub (Canavaro) kwa kufanya makosa kadhaa ambayo yamesababisha washambuliaji wa Mtibwa Sugar kupata mabao matatu mawili yakipachikwa nyavuni Hussein Javu na Dickson Daud kufunga bao hizo.
Omari alisema kuwa bao la kwanza lililofungwa na kichwa na Dickson Daud katika dakika 11 mfungaji huyo aliruka juu pekee yake na kufungwa kufuatia mpira wa kona uliochongwa na Maliki Ndeuka.
“Ule ni uzembe wa mabeki wetu kwani ukiangalia bao la kwanza mfungaji alikuwa pekee yake hakubugudhiwa hata kitogo na hata mabao mawili yaliyofungwa na Hussein Javu ni makosa yao wenyewe walinzi pale huwezi kumlaumu mlinda mlango hata kidogo” alisema Omari.
Aliongeza kuwa mabao mawili ya Hussein Javu aliyopachika wavuni dakika ya 44 na 76 yote yametokana na uzembe wao walinzi ambapo aliyafungwa nje ya 18 na kumshinda mlinda mlango namba mbili wa klabu hiyo ya Yanga Ally Mustafa (Bathez).
Naye Jackson Tesha alisema kuwa kikosi cha Yanga kilichocheza na Mtibwa Sugar hakikuzingatia umuhumu wa timu husika kama Mtibwa Sugar ambayo miaka mingi imekuwa ikifungwa katika michezo mbalimbali ya mashindano na kirafiki.
Tesha alisema kuwa baadhi ya wachezaji walicheza sehemu ambazo kiujumla hawakuweza kuzimudu kuzicheza tofauti na zile ambazo wamekuwa wakicheza kwa kiwango kilichozoeleka katika michezo iliyopita.
Kati ya Mbuyu Twite na Kelvin Yondani mmoja wao angeweza kuanza kikosi cha kwanza na mungine akitokea benchi katika mchezo Mbuyu Twite amekuwa akimudu sehemu ya ulinzi namba nne na tano lakini mchezo wa jana alicheza tatu huku Kelvin Yondani akichezeshwa katika sehemu ya ulinzi namna nne tofauti na namba tano ambayo anamudu zaidi.
Wakati mlinzi Juma Abdul hakuwa katika kiwango chango chake hivyo kuwa sehemu ya mwaya kwa wachezaji wa Mtibwa Sugar kupitia huo kwa mashambulizi.
0 comments:
Post a Comment