BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BONDIA FRANCIS CHEKA (SMG) AMTWANGA CHIMWEMWE KATIKA UKUMBI WA SHEKHE AMRI ABEID JIJINI ARUSHA. ATETEA TAJI LA IBF AFRIKA.


KWA UFUPI
Raundi ya nne, tano, sita na saba Cheka alianza cheche zake kwa kushambulia mfululizo hali iliyoamsha furaha kwa mashabiki wake, ambao awali walionekana kukaa kimya.Bondia Francis Cheka akivishwa mkanda wa ubingwa wa IBF na Meya wa jiji la Arusha, Gaudence Lyimo (kushoto) na rais wa TPBC Onesmo Ngowi baada ya kumtwanga mpinzani wake Chotka Chimwemwe wa Malawi kwa pointi katika pambano lililofanyika kwenye  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, Arusha. Picha na rockersports.blogspot.com.
FRANCIS Cheka amemtwanga mpinzani wake, Chiotra Chimwemwe kutoka Malawi na kutetea vyema mkanda wake wa IBF Afrika.
Cheka alimshinda mpinzani wake kwa pointi katika pambano la raundi 12 uzito wa Super middle kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini hapa.
Pamoja na ushindi huo Cheka atalazimika kushonwa nyuzi tatu kwa mujibu wa daktari wake, Brown Lubeni baada ya ngumi ya Chimwemwe ya raundi ya pili kumpasua paji la uso hivyo kucheza raundi zote 12 akiwa anavuja damu.
Mwamuzi wa pambano hilo, George Kavishe alilazimika kusimamisha pambano mara kadhaa ili Cheka atibiwe kufuatia kuvuja damu mfululizo kwenye paji la uso alipopasuliwa.
Katika mchezo huo, Cheka alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa Chimwemwe, ambapo hadi raundi ya mwisho siyo Cheka wala Chimwemwe aliyekuwa amejihakikishia ushindi.
Kabla ya kuanza kwa pambano hilo lililovuta hisia za mashabiki wengi waliompa nafasi ya ubingwa Cheka, mambo yalikuwa kinyume chake kwani mashabiki walilazimika kusubiri mpaka mwisho kufahamu nani bingwa.
Cheka alikuwa wa kwanza kupanda ulingoni, akisindikizwa na wapambe wake akitokea upande wa nyuma wa uwanja na dakika tatu baadaye Chimwemwe alipanda ulingoni.
Chimwemwe ndiye alianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumwangusha Cheka chini katika raundi hiyo na kuwapa furaha mashabiki wake wachache waliokuwa hapo.
Raundi ya pili ilikuwa tete kwa Cheka, ambaye aliporomoshewa makonde mfululizo hali iliyosababisha mashabiki wake kuonekana kukata tamaa.
Hata hivyo dakika ya pili ya raundi ya tatu Cheka alibadilika na kuanza kushambulia, huku akijihami kutokana na kupasuliwa raundi ya pili kwa konde.
Raundi ya nne, tano, sita na saba Cheka alianza cheche zake kwa kushambulia mfululizo hali iliyoamsha furaha kwa mashabiki wake, ambao awali walionekana kukaa kimya.
Chimwemwe licha ya kushambuliwa kwenye raundi nane, tisa, kumi, kumi na moja, alijitutumua na kufanya mashambulizi ya kushtukiza raundi za mwisho.
Baada ya pambano hilo Cheka aliyejikuta akivuja damu muda wote alisema, mchezo ulikuwa mgumu na kusisitiza hajawahi kuona bondia mbishi kama Mmalawi huyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: