BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM YAPANIA KUINGIA JIMBO LA KARATU KWA NGUVU.

KWA UFUPI:
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imejipanga kuwasaidia vijana lakini haiwezekani kusaidia mtu mmoja mmoja hivyo mnapaswa kuunda vikundi na tutashirikiana mpate maeneo ya ujasiriamali na pia vitalu vya kuchimba madini ya dhahabu ambayo yamegundulika hapa Karatu,”alisema AwakieNape Nnauye akifafanua jambo kwa msisitizo.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa Wilaya ya Karatu, Daniel Awakie, amewataka vijana wilayani Karatu, kuungana na kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na uchimbaji madini, ili iwe rahisi kusaidiwa na Serikali.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kata za Karatu mjini na Qasai, katika mfululizo wa mikutano yake ya kukagua uhai wa chama hicho, Awakie alisema ili vijana waweze kupata usaidizi ni vyema wakaungana.
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imejipanga kuwasaidia vijana lakini haiwezekani kusaidia mtu mmoja mmoja hivyo mnapaswa kuunda vikundi na tutashirikiana mpate maeneo ya ujasiriamali na pia vitalu vya kuchimba madini ya dhahabu ambayo yamegundulika hapa Karatu,”alisema Awakie
Awakie alisema Serikali ya CCM imejipanga kutatua kero za wananchi wa Karatu, ili kuhakikisha pia kuwa wanalirejesha CCM Jimbo la Karatu ambalo kwa sasa linashikiliwa na Chadema.
“Ndugu zangu tumewapa Chadema jimbo na halmashauri, lakini wameshindwa kutatua matatizo yetu, sasa wapo katika mgogoro, tumekuja hapa kuwaeleza kuwa CCM inakusudia kuondoa kero zetu,”alisema Awakie.
Alisema CCM sasa imepania kurejesha heshima yake Karatu, kwa kuwa karibu na wananchi na kupokea kero zao na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Karatu, Mustapha Kassimu ,alisema katika kuhakikisha kuwa wanarejesha jimbo hilo, wanatarajia kushinda katika uchaguzi wa mji mdogo Karatu.
“Tunataka tuanze na uchaguzi wa mji mdogo, kwani hapa mjini kuna matatizo ya vijana kukosa maeneo kwa wajasiriamali na viongozi wa Chadema wameshindwa kuwasaidia na kuamua kuwaondoa mjini. Sasa CCM tumesema wasiondoke mpaka wapewe maeneo,”alisema Kassim.
Katika mikutano hiyo, baadhi ya vijana waliutaka uongozi wa CCM kusaidia kupata maeneo ya kufanya biashara zao hasa baada ya kutakiwa kuondoka katikati ya mji wa Karatu/
Pia walitaka wasaidiwe kupata leseni za kuchimba madini ya dhahabu yaliyogundulika katika Kata ya Endabash, wilayani humo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: