KWA UFUPI
Askari polisi huyo ambaye hakutaka jina lake
litajwe, kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo alisema kwamba, wakati
dereva huyo akiwa ameshuka chini, ghafla lilianza kurudi nyuma, “Ilibidi
arukie na kwenda kukanyaga breki, lakini ikashindikana na basi hilo
likatumbukia kwenye korongo na kupinduka mara tatu,” alisema askari
huyo.
BASI LA USOKOMI TOURS MARA BAADA YA KUPATA AJALI MKOANI IRINGA.
WATU tisa wamefariki dunia na wengine 61 kujeruhiwa baada ya
basi walilokuwa wakisafiria mkoani Iringa, kupata hitilafu ya breki na
kutumbukia kwenye korongo.
Ajali hiyo ilitokea saa 8 mchana jana katika eneo la Mlima Ihemi, Wilaya ya Iringa Vijijini, ikihusisha basi la abiria maarufu kwa jina la Usokomi Tours.
Ajali hiyo ilitokea saa 8 mchana jana katika eneo la Mlima Ihemi, Wilaya ya Iringa Vijijini, ikihusisha basi la abiria maarufu kwa jina la Usokomi Tours.
Basi hilo lilikuwa likitokea Iringa mjini kuelekea Kijiji cha Usokomi wilayani Mufindi.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk Faustine Gwanchele alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu hao na majeruhi na kuongeza kuwa, maiti zimehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali hiyo.
Dk Gwachele alisema kuwa, alipokea maiti tisa, zote zikiwa ni za wanawake ambapo sita zilitambuliwa.

Alisema kuwa, kati ya majeruhi 61 waliofikishwa
hospitalini hapo na kutibiwa, 33 waliruhusiwa huku 28 wakilazwa, baada
ya hali zao kuonekana zinahitaji matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa mmoja wa askari polisi waliokuwa kwenye eneo la tukio, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva kuliegesha gari hilo wakati wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuruhusiwa wapite kutokana na barabara hiyo kuwa kwenye ujenzi.

Alisema kuwa, dereva wa gari hilo alishuka akifikiri kondakta wake ameweka kizuizi kwenye tairi, ili kulizuia lisirudi nyuma.
Askari polisi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo alisema kwamba, wakati dereva huyo akiwa ameshuka chini, ghafla lilianza kurudi nyuma.
“Ilibidi arukie na kwenda kukanyaga breki, lakini ikashindikana na basi hilo likatumbukia kwenye korongo na kupinduka mara tatu,” alisema askari huyo.
Alisema basi hilo lina uwezo wa kubeba abiria 64, lakini inaelekea lilikuwa na idadi kubwa zaidi ya hao, wakiwa wamesongamana.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, Mchungaji John
Mwakione, ambaye alitibiwa na kuruhusiwa alizilaumu mamlaka za usimamizi
barabarani kwa kushindwa kuwa makini.
Desemba 3, ajali nyingine ilitokea eneo la Tanangozi mkoani humo na kusababisha vifo vya watu watano, wanne wakiwa wa familia moja .
Desemba 3, ajali nyingine ilitokea eneo la Tanangozi mkoani humo na kusababisha vifo vya watu watano, wanne wakiwa wa familia moja .
Ajali hiyo ilitokea saa nane mchana wilayani
Iringa katika kizuizi cha barabara ambapo unafanyika ukarabati wa
Barabara Kuu ya Iringa - Mafinga mkoani Iringa.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba
chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuligonga
kwa nyuma lori lililokuwa na tela kwa nyuma, ikielezwa kuwa dereva wa
gari hilo alikuwa katika mwendo wa kasi ambapo alishindwa kulimudu,
ndipo lilipoligonga lori hilo.
Ajali hiyo ilipoteza maisha ya Ezekiel Mwaiteleke,
mkewe, watoto wake wawili na mfanyakazi wao waliokuwa wakitokea Dar es
Salaam, kwenda Kyela mkoani Mbeya,ambao walifariki papohapo na maiti
zote kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
0 comments:
Post a Comment