Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema
Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia
matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth
Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.Picha na
Freddy Maro
Mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru
kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema
aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.
Kwa apande wake ,Mama
Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na
vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye
waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
0 comments:
Post a Comment