Kwa ufupi:
Alisema hata ikitokea kweli askari aliyepiga naye
picha akafukuzwa kazi hatajuta kumsababishia madhila hayo bali
atajisikia faraja kwa sababu kitendo hicho kitafungua ukurasa mpyae
katika harakati za ukombozi kwa watu kuelewa kuwa siyo kila jaribu au
makosa ni mkosi, bali ni hatua muhimu katika kufikia mafanikio ya
unachokiamini.
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania
(JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema
(Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya
kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji
mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara.
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema kama
angekuwa ndiye mwenye uamuzi ya mwisho ndani ya Chadema, angempokea
kwenye chama hicho askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
aliyepiga naye picha kama kitendo hicho kitamfanya afukuzwe kazi.
“Ingawa wanaofaa kutoa kauli kama hizi ni viongozi
wakuu kama Mwenyekiti na Katibu wa Taifa kupitia vikao halali vya
chama, lakini binafsi, ningekuwa na uwezo, ningempokea mara moja askari
huyu kwenye chama kama ishara ya walio tayari kujitoa mhanga kupoteza
vyote ikiwemo kazi kwa ajili ya ukombozi wa taifa iwapo atafukuzwa
kazi,” alisema Lema.
Hata hivyo, Lema aliyekuwa akizungumza katika
mahojiano maalumu akiwa mjini Moshi kwa mapumziko ya Sikukuu ya
Krismasi, alisema kitendo cha JWTZ kuanza kumwandama na pengine
kumfukuza kazi askari huyo, kitafumua chuki kubwa kati ya askari wa vyeo
vya chini na wenye vyeo vya juu ambao wengi wanaitumikia CCM kwa nafasi
zao, ukiwemo ukuu wa mikoa na wilaya.
Alitoa mfano Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Samuel Ndomba
ambaye kabla ya kuhamishiwa Makao Makuu ya jeshi alikoshika nyadhifa
mbalimbali na hatimaye kuteuliwa kushika nafasi yake ya sasa, alikuwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, cheo kilichompa fursa ya kuwa mjumbe wa
Halmashauri Kuu na Kamati ya siasa mkoa wa CCM, Mkoa wa Arusha.
“Askari huyu mdogo akifukuzwa kazi kwa sababu ya
picha aliyopiga na sisi, basi itathibitisha double standard (undumila
kuwili) ya utawala katika taifa letu. Huyu kapiga picha na taarifa ya
kusakwa inatolewa na JWTZ , lakini wako wengi ambao ni wanajeshi wa vyeo
vya juu ambao siyo tu wanapiga picha na viongozi wa chama tawala bali
ni wafanyakazi wa CCM kwa nyadhifa zao wakiwa bado wako jeshini,”
alisema Lema.
Alisema ujasiri wa mtu huyo anayeamini kuwa kweli
ni askari wa JWTZ kujitokeza kupiga naye picha huku akijua anahatarisha
kazi yake, ni ushahidi kuwa wapo askari wengi nchini waliochoshwa na
mwenendo wa CCM.
Alisema ukweli huo unathibitishwa na matokeo ya
kura katika vituo vilivyokuwa ndani au jirani na vituo vya polisi na
kambi za jeshi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo wagombea wa
upinzani walipata kura nyingi ikilinganishwa na wale wa CCM.
Lema aliyepiga picha na askari huyo akiwa na
mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), alitoa
changamoto kwa watu wenye mapenzi mema na taifa hili, kufanya utafiti wa
maofisa wa juu wa JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
wanaotumikia chama tawala kwa siri au kwa uwazi kupitia vyeo na nyadhifa
zao.
“Hawa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM ambao tunashuhudia wakirejea jeshini wakitokea kwenye utumishi wa chama lakini hatujawahi kusikia tamko la kutafutwa wala kuchunguzwa na jeshi kwa kushiriki siasa,” alisema Lema.
“Hawa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM ambao tunashuhudia wakirejea jeshini wakitokea kwenye utumishi wa chama lakini hatujawahi kusikia tamko la kutafutwa wala kuchunguzwa na jeshi kwa kushiriki siasa,” alisema Lema.
Alisema hata ikitokea kweli askari aliyepiga naye
picha akafukuzwa kazi hatajuta kumsababishia madhila hayo bali
atajisikia faraja kwa sababu kitendo hicho kitafungua ukurasa mpyae
katika harakati za ukombozi kwa watu kuelewa kuwa siyo kila jaribu au
makosa ni mkosi, bali ni hatua muhimu katika kufikia mafanikio ya
unachokiamini.
Alisema askari huyo atakuwa ameshinda hofu,
vitisho na uoga alivyosema ni miongoni mwa dhambi kuu katika maisha ya
mwanadamu na kuwataka Watanzania kutoogopa lolote, hata ikibidi kifo
wakati wakipigania haki zao kwani hakuna atakayeishi milele kwa kuogopa
kufa.
“Ni heri mtu kuishi miaka michache duniani na Jina
lake kubaki linaishi kwa haki na wema kuliko kuishi miaka mingi
akatoweka kama mzoga” alisema Lema akimkariri Mwana mapinduzi Steve Biko
na kuongeza “Ni dhambi kubwa katika demokrasia kuupuuza ukweli eti kwa
sababu anayesema uongo amejifunza kupiga na kuua,”
Lema aliishauri JWTZ kutekeleza ahadi ya kulinda
Taifa hata kwa kukemea kwa maneno wizi wa mali na rasilimali za umma
zikiwemo fedha na wanyapori wanaotoroshwa kwenda nje kwa msaada wa
waliokabidhiwa dhamana ya kuvilinda na kuvitunza kwa faida ya wote.
0 comments:
Post a Comment