Kwa ufupi
“Leo hii waziri ananipigia simu kuniuliza mahitaji
yetu ni yapi, hilo ni jambo la msingi ndiyo maana nasema tamko
lililotolewa wakati wa maandamano ni dhaifu kwa sababu halielezi
mahitaji yetu ni yapi. Lazima tuwape conditions (masharti) kwamba gesi
ikienda Dar es Salaam sisi tunahitaji hiki na kile,” alifafanua Murji.
BAADA ya kutoonekana kwenye maandamano ya wakazi wa Mkoa wa
Mtwara ya kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam yaliyofanyika Desemba 27
mwaka huu, Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji ameibuka na kusema
anaunga mkono wananchi hao kutetea maslahi yao na kuwa tamko
lililotolewa lilikuwa dhaifu.
“Hoja ya msingi ni kwa namna gani bomba la gesi
litanufaisha Wana-Mtwara. Mimi kwa kiwango fulani sikubaliani na hoja ya
gesi isiende Dar es Salaam lakini naungana na wananchi kudai
tutafaidikaje na bomba hilo,” alisema Murji katika mahojiano maalumu na
mwandishi wa habari hizi jana.
Alisisitiza kuwa, “Ninakubali gesi iende Dar es
Salaam kwa sharti la kuzalisha umeme tu, si kwa matumizi mengine,
wakianza kuitumia kwenye viwanda watakuwa wametuua kabisa.”
Alibainisha kuwa kitendo cha wananchi kuandamana ni haki yao ya msingi na hakipaswi kubezwa na mtu yeyote kwa sababu wanateteta haki yao ya msingi ya kufaidika na rasilimali yao.
Alibainisha kuwa kitendo cha wananchi kuandamana ni haki yao ya msingi na hakipaswi kubezwa na mtu yeyote kwa sababu wanateteta haki yao ya msingi ya kufaidika na rasilimali yao.
“Leo hii waziri ananipigia simu kuniuliza mahitaji
yetu ni yapi, hilo ni jambo la msingi ndiyo maana nasema tamko
lililotolewa wakati wa maandamano ni dhaifu kwa sababu halielezi
mahitaji yetu ni yapi. Lazima tuwape conditions (masharti) kwamba gesi
ikienda Dar es Salaam sisi tunahitaji hiki na kile,” alifafanua Murji.
Aliongeza kuwa, “Nimeandaa kikao na viongozi wa
umoja wa vyama vya siasa vilivyoratibu maandamano hayo ili tukae
tuainishe mahitaji yetu ni yapi iwapo gesi itakwenda Dar es Salaam,
lazima tuwe na mkataba, tusikatae tu, tueleze tunahitaji nini gesi
ikienda Dar es Salaam.
Akizungumzia kauli ya mkuu wa mkoa huo, Joseph
Simbakalia ya kuwaita wanaopinga gesi kupelekwa Dar es Salaam wapuuzi na
baadaye wahaini, Murji alisema “Hakupaswa kufanya hivyo, si busara
kuwaita watu wanaodai haki yao wapuuzi au wahaini.”
Alieleza kuwa ni vyema angekwenda kupokea
maandamano na baadaye angewaelimisha wananchi waliokuwapo hapo kuwa
Serikali imeamua hivyo kwa sababu kadhaa. Wapo ambao wangemwelewa,
lakini kuwaita wapuuzi au wahaini sidhani kama itasaidia.”
Kauli hiyo ya mbunge imekuja wakati ambapo tayari
Mkuu wa mkoa huo Simbakalia amesisistiza kuwa alikuwa sahihi kuwaita
wapuuzi na pengine wahaini, huku Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo akikazia uzi kuwa walioandaa maandamano hayo ni watu
hatari kwa usalama wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment