BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGEJA: SERA ZA CHADEMA ZIPUUZWE


KWA UFUPI.
Pia, alisema Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa ,aliwahi kukaririwa akitamka kuwa baadhi ya sera zinazotekelezwa na CCM, walizinakiri kutoka kwao, “Kutoa mawazo na kusimamia hoja ni mambo mawili tofauti, hayapishani na mchangia harusi asiyekuwa na uwezo wa kuoa,” alisema Mgeja.
NAPE NNNAUYE KUSHOTO NA KHAMIS MGEJA KULIA



MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja amewataka Watanzania kupuuza sera za upinzani na kuzifananisha kama mchangia harusi ambaye hana uwezo wa kuoa.

Akihutubia wakazi wa Kata ya Nyankende, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Mgeja alisema Watanzania hawanabudi kupuuza porojo za wapinzani, kwa sababu haziwasaidii.

Mgeja alisema wapinzani wamekuwa na propaganda nyingi, huku wakibeza CCM kuwa haijafanya chochote kwa miaka 51 ya uhuru.

Pia, alisema Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa ,aliwahi kukaririwa akitamka kuwa baadhi ya sera zinazotekelezwa na CCM, walizinakiri kutoka kwao.

“Kutoa mawazo na kusimamia hoja ni mambo mawili tofauti, hayapishani na mchangia harusi asiyekuwa na uwezo wa kuoa,” alisema Mgeja.

Mgeja aliwataka wananchi wa Shinyanga na watanzania kuepuka maneno yanayotolewa na viongozi wa vyama hivyo, kwani vitawavuruga, kuwachanganya na kupotosha fikra za CCM.

Alisema watu hao siyo waungwana na ndiyo maana wanabeza mafanikio ya CCM.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: