MWILI wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore
baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi utarejeshwa kwa ndege maalum
ya kukodi baadaye leo Jumamosi.
Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu watasafirishwa kwenda India katika ndege maalum ya kukodi baadaye mchana wa leo Jumamosi, amesema Raghavan.
Waziri mkuu ahuzunika
Waziri mkuu wa india Manmohan Singh amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mwanamke huyo ambaye alifanyiwa vitendo vya kinyama kwa kubakwa na kundi la vijana na kwamba maandamano yaliyozuka kutoka na kitendo hicho , "yanaeleweka".
Wanawake wakiandamana nchini India wakipinga matumizi ya nguvu katika ngono.
ameandika waziri huyo mkuu katika tovuti yake.
"Tumekwisha ona hisia na nguvu ambazo tukio hili limesababisha. Hii ni hali ambayo inaeleweka kutoka kwa vijana wa india ambao wanataka mabadiliko ya kweli.
"Nataka kuwaambia , familia yake na taifa kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure."
Waziri mkuu wa India Manmohan Singh.
Serikali imekuwa ikijaribu kulituliza wimbi la hasira kwa kuahidi adhabu kali kwa uhalifu mkubwa unaohusiana na ngono pamoja na kuunda tume maalum ya uchunguzi kuhusiana na jinsi ya kushughulikia kesi za ubakaji.
Polisi wautaka umma kuomboleza kwa amani
Wakati maafisa wakijitayarisha kwa ghasia zaidi mitaani, polisi wameonekana kuongezwa katika eneo la kati la mji mkuu wa india kabla ya mwili wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 haujarejeshwa nchini humo.
Afisa wa polisi wa mjini New Delhi amehimiza watu kuomboleza kifo cha mwanamke huyo kwa amani wakati maeneo kadha ya mji huo mkuu yamefungwa.
Polisi wanajiandaa kwa maandamano makubwa zaidi nchini India
Singh , ambaye hapo kabla alitoa wito wa utulivu , amesema kuwa
itakuwa , "Heshima kubwa kwa kumbukumbu yake iwapo tutaweza
kuelekeza hisia zetu hizi na nguvu katika kuchukua hatua sahihi.""Kwa muda huu tunahitaji mjadala wa maana na uchunguzi kuhusiana na mabadiliko ya lazima na haraka ambayo yanahitajika katika mtazamo wa jamii.
"Ni matumaini yangu kuwa tabaka lote la kisiasa pamoja na jamii yote itatenga maslahi yao finyu ya binafsi na ajenda ili kutusaidia kufikia hatima ambayo tunaikusudia, na kuifanya india kuwa mahali bora na salama kwa wanawake kuweza kuishi.
0 comments:
Post a Comment